LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 10, 2024

RAIS DK. SAMIA AAPISHA VIONGOZI KUHUDUMU NAFASI MPYA, IKULU NDOGO YA TUNGUU, ZANZIBAR, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, leo, Disemba 10, 2024.
Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi.
Mhandisi Maryprisca Winfried Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Hamis Mohamed Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Dkt. James Henry Kilabuko kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Dkt. Stephen Justice Nindi, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji).
Anderson Gukwi Mutatembwa kuwa Balozi.
Mobhare Holmes Matinyi kuwa Balozi.
Kamishna wa Polisi Hamad Khamis Hamad kuwa Balozi.
Kamishna wa Polisi Suzan Salome Kaganda kuwa Balozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la uapisho katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, leo Disemba 10, 2024.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages