LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 11, 2024

MAJENGO TULIYOYAJENGA MJI WA KISERIKALI NI YA VIWANGO- MWENYEKITI WA BODI NHC

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakiongozwa na Mwenyekiti, Dkt. Sophia Kongela  (wa pili kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo yanayojengwa na shirika hilo kwenye Mji wa Kiserikali Mtumba Makao Makauu ya Nchi Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Hamad Abdallah.

Majengo manne kati ya 10 yanayotekelezwa na shirika hilo yaliyokaguliwa ni ya Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mhandisi Anthony Sanga akiipongea bodi na menejimenti ya shirika hilo kwa ujenzi bora wa majengo hayo likiwemo la wizara hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Dkt. Kongela amesema kuwa ameridhishwa na kanzi nzuri inayofanywa makandarasi na wafanyakazi wa shirika hilo kwa kujenga majengo yenye viwango.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Hamad Abdallah akiwaonesha wajumbe wa bodi maendeleo ya ujenzi huo.
Abdalah akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga kuhusu mikakati wanayoifanya kuhakikisha ujenzi unakamilika mapema.

Wajube wa Bodi wakikagua maeneo mbalimbali.

Moja vya vyoo vilivyokamilika.
Wakiangalia moja ya majiko yaliyopo katika majengo hayo.



 

Kazi ikiendelea ya kusafisha baadhi ya maeneo ambayo ujenzi wake umekamilika.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages