Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kwa kurejesha mawasiliano ya barabara Kuu ya Manyara - Singida ambayo iliathirika Desema 3, 2023 wakati wa maafa ya maporomoko ya tope la mlima Hanang Mkoani Manyara.
Akizungumza Desemba 20,2024 wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope zilizojengwa katika kitongoji cha Waret, kijiji cha Gidagamowd wilayani Hanang mkoani Manyara Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imefarijika kwa jitihada za zilizofanywa na Wizara kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea kama ilivyokuwa awali.
“Niwapongeze Wizara ya Ujenzi, nakuona Mheshimiwa Kasekenya upo hapa, mlifanya kazi nzuri na ya kupongezwa kuhakikisha barabara hii inarejea vizuri”, amesema Majaliwa
Katika hafla hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amezindua na kukabidhi jumla ya hati za nyumba 109 ambapo Nyumba 73 zimejengwa na Serikali kwa kuputia SUMA JKT, 35 zimejengwa na RED CROSS na moja imejengwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).
Aidha, mbali na kukabidhi hati, pia amekabidhi majiko 109 ya nishati safi ya kupikia ambayo ni zawadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waathirika hao.
Muonekano wa nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope zilizojengwa katika kitongoji cha Waret, kijiji cha Gidagamowd wilayani Hanang mkoani Manyara.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizindua nyumba hizo. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhadisi Godfrey Kaekenya (wa pili kulia) akikagua miundombinu ya barabara katika eneo hilo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇