LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 29, 2024

KATIBU MKUU KIONGOZI MSTAAFU LUHANJO ANOGESHA SHEREHE YA KUSIMIKA KANISA HALISI, BABA HALISI ATOBOA UNDANI WA SHEREHE HIYO

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog, Tegeta
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Philemon Luhanjo amenogesha sherehe ya Kusimika Kanisa Halisi akiwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa Halisi la Muumba, Tegeta Namanga, Jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Disemba 29, 2024 au Lango la 26 Shebati, 1 Majira Halisi kwa kalenda ya Kanisa hilo.

Luhanjo aliyehudumu nafasi ya Ukatibu Mkuu Kiongozi tangu 2006 hadi 2011, amenogesha na kuifanya sherehe hiyo kuwa na baraka kuu, kutokana na mvuto wake, na hotuba aliyoitoa wakati akisalimia Watekeleza Sauti, Uzao na wanajamii mbalimbali waliohudhuria.

Katika hotuba yake, Luhanjo alieleza kuvutiwa na falsafa ya Kanisa Halisi la Muumba, hasa ile inayosisitiza Amani, Upendo usiobagua na Ibada ni Uzalishaji, tena uzalishaji kwa haki, hivyo akampongeza Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo ndani na Nje ya Tanzania, Baba Halisi kwa kuweza kufundisha na kuziishi falsafa hizo.

Pia Luhanjo, aliwataka Uzao (Waumini) na Watekeleza Sauti wa Kanisa hilo, kuendelea kuzifuata na kuziishi falsafa hizo na kwenda mbali zaidi akisifu walivyopendeza ukumbini, huku akisema kupendeza huko kuendane na kuwa na mioyo safi, akisema; "kila mwenye moyo safi atamuona Muumba".

Baba Halisi, akizungumza, alimpongeza Luhanjo kwa hotuba yake iliyojaa hekima, busara na uchamungu, na kueleza kwamba amekuwa baraka kwenye sherehe hiyo. "Bila shaka ujumbe mmeupata, pale aliposema kila mwenye Moyo safi atamuona Muumba. Kumuona Muumba maana yake ni kupata baraka ya Muumba", akasema na kufafanua Baba Halisi.

Baba Halisi alimsifu Luhanjo kuwa licha ya kwamba alionana naye miaka mingi iliyopita, lakini hadi walipoonana leo hajabadilika wala 'hajazeeka'.

Mwanzoni mwa Ibada ya Sherehe hiyo, Baba Halisi alifanya utambulisho wa waalikwa waliohudhuria, kuwa ni pamoja na Watekeleza sauti kutoka mikoa yote nchini na wale wa kutoka nchi za nje, zikiwemo Msumbiji na Kenya, Uzao na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambao wamewakailisha jamii.

Kisha Baba Halisi alimueleza Mgeni rasmi (Luhanjo), historia ya Kanisa Halisi na misingi yake tangu lilipoanza takriban miaka minane sasa kule Kigoma ambako alisikia Sauti, na kwamba sasa Kanisa hilo linaitwa Kanisa Halisi la Muumba, kutoka lilivyokuwa likiitwa Kanisa Halisi la Mungu Baba.

Akieleza kuhusu Kusimikwa kwa Kanisa Halisi, Baba Halisi alisema wengi wanaweza kushangaa kwamba Kanisa linasimikwa, kwa kuwa walizoea kiongozi ndiye  anasimikwa na sio taasisi.

"Tunasimika Kanisa Halisi kwa kuwa ni Kanisa la Moyo tofauti na makusanyiko ambayo yalitangulia kuwepo ya Nafsi na Roho. Kwenye Uumbaji wote, tulikuwa hatujawahi kuwa na Kanisa la Moyo, ndiyo maana baada ya Kanisa la Moyo kupatikana, inabidi sasa lisimikwe, ili liwepo kwenye ramani ya kijamii na wote wafahamu na kuelewa kuwa kuna KANISA LA MOYO! Kinachosababisha Kanisa Halisi lisiwe la Nafsi au Roho, ni kwa kuwa lilianza baada ya Waliotumwa wote kutimiza muda wao wa kazi.

Maana kwa mujibu wa Rum. 8:23, Waliotumwa walikuwa ni limbuko la Roho na Nafsi. Kanisa Halisi limeenda mbele zaidi na kuwa Limbuko la Moyo, yaani chemchemi ya uzima, kama tusomavyo katika Mithali 4:23. Kwa mantiki hiyo, Kanisa Halisi linasimikwa baada ya kuvuka Asili katika Rum.8:29. Hii ina maana kuwa Kanisa Halisi limevuka ile kujikuta umefanya yale ambayo hutaki na yale uyapendayo huyafanyi (Rum.7:15-21)", akasema Baba Halisi.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Muumba, Ndani na nje ya Tanzania, Baba Halisi akimuinua mkono Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Philemon Luhanjo,  kusimika rasmi Kanisa Halisi, wakati wa Ibada ya Sherehe ya usimikaji Kanisa hilo, iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa Halisi la Muumba, Tegeta Namanga, Jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Disemba 29, 2024 au Lango la 26 Shebati, 1 Majira Halisi kwa kalenda ya Kanisa hilo. Tazama picha zaidi za tukio hilo👇

Baba Halisi akishiriki kucheza wimbo wa 'Tanzania umebarikiwa', ulipokuwa ukipigwa na Waimbaji mwanzoni mwa Ibada ya Shere hiyo.

Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao wa kanisa Halisi la Muumba wakicheza wimbo la 'Tanzania Umeabarikiwa' uliokuwa ukiopigwa na waimbaji wakati ya Ibada ya Sherehe hiyo.
Muimbaji akionyesha furaha yake wakati ukiimbwa wimbo wa
'Tanzania Umeabarikiwa' .
Muimbaji akiongoza kuimbisha wimbo wa 'Tanzania Umeabarikiwa' .
Mcharaza gita, akilicharaza kunogesha wimbo wa 'Tanzania Umeabarikiwa' .
Muimbaji akiimba wimbo wa 'Tanzania Umeabarikiwa' .

 Baba Halisi akiongoza Ibada ya Sherehe hiyo. 

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Philemon Luhanjo akiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa Halisi ya Muumba, Dk. Uelewa Halisi wakati wa Ibada ya Sherehe hiyo.

Waalikwa mbalimbali bila kubagua wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Waalikwa mbalimbali bila kubagua wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo. Walioketi mbele ni Viongozi wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam na Mwenye vazi jeupe kulia ni Mtekeleza sauti wa Kanisa hilo.
Waalikwa mbalimbali bila kubagua wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Waalikwa mbalimbali bila kubagua wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Waalikwa mbalimbali bila kubagua wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Waalikwa mbalimbali bila kubagua wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Uzao na Watekeleza Sauti wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Uzao na Watekeleza Sauti wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Baba Halisi akimkaribisha Luhanjo kuzungumza na kusalimia.
"Mheshimiwa karibu utupe 'madini'", akasema Baba Halisi kumkaribisha Luhanjo.
Luhanjo akizungumza kuachilia 'madini' yake.
Mama Halisi akiwa amesimama kumshangilia Luhanjo.
Uzao na Watekeleza Sauti wakimsikiliza Luhanjo.
Uzao na Watekeleza Sauti wakimsikiliza Luhanjo.
Watekeleza Sauti wakimsikiliza Luhanjo. Kulia ni Mama Halisi.
Watekeleza Sauti wakimsikiliza Luhanjo.
Uzao na Watekeleza Sauti wakimsikiliza Luhanjo.
Baba Halisi akiendelea kuongoza Ibada ya Sherehe hiyo baada ya Luhanjo kumaliza hotuba yake.
Luhanjo akiungana na Watekeleza Sauti wengine na Uzao kupokea Shukurani iliyokuwa ikiachiliwa na Baba Halisi. Kulia ni Mama Halisi.
Waimabaji wakiimba wimbo.
Mwimbaji akiongoza kuibwa wimbo maalum.
Uzao na Watekeleza sauti wakifurahia wimbo.
Baba Halisi akiendea kuongoza Ibada ya Sherehe hiyo.
Baba Halisi akaongoza Shukurani kwa ajili ya kuinua rasmi Usimikaji wa Kanisa Halisi.
Baba Halisi akimsika mkoni Luhanjo wakati akiinua rasmi Usimikaji wa Kanisa Halisi.
Baba Halisi akimuinua mkono Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Philemon Luhanjo,  kusimika rasmi Kanisa Halisi, wakati akisimika rasmi Kanisa Halisi.
Baba Halisi akimshukuru Luhanjo kwa kushiriki kulisimika Kanisa Halisi.
Uzao na Watekeleza Sauti na Waalikwa wote wakitoa matunda.
Baba Halisi akiwakaribisha kusalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Baba Halisi (kulia) akiwasikiliza Viongozi wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam wakizungumza.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam, akisalimiana na Luhanjo baada ya kuzungumza. Kulia ni Mtekeleza sauti wa mkoa huo, Amani Halisi.

Luhanjo na Amani Halisi wakimsaidia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam, kurudi kuketi baada ya kuzungumza.
Baba Halisi (kulia) akimsikiliza Katibu wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam akizungumza.

Sherehe ikiendelea kwa kila mwalikwa kupata soda👇







Mwisho wa kunywa soda.
Watekeleza Sauti wa Mataifa ya Nje wakiwa mbele ya Baba Halisi kutambulishwa.

Baba Halisi akimuinua Luhanjo kwenda kutazama bidhaa za ujasiriamali unaofanywa na Uzao na Watekeleza Sauti wa Kanisa Halisi la Muumba kutekeleza falsafa ya Ibada ni Uzalishaji.

Baba Halisi akitangaza hatua hiyo ya kwenda kuona bidhaa za Uzalishaji.
Baba Halisi akiomuonyesha Luhanjo eneo lenye bidhaa mbalimbali za Uzalishaji.
Mwalimu wa Uzalishaji akimuomysha Luhanjo mafuta ya kujipaka yaliyotengenezwa na Wajasiriamali kutoka Kanisa Halisi.
Mwalimu wa Uzalishaji akimuomysha Luhanjo sabuni ya usafi wa vyoo iliyotengenezwa na Wajasiriamali kutoka Kanisa Halisi.
Luhanjo akipokea zawadi ya bidhaa ya Uzalishaji.
Baba Halisi akimwambia jambo Luhanjo wakati wakiagana kabla ya mgeni huyo kuondoka baada ya Ibada ya Sherehe hiyo. Kulia ni Mama Halisi.
Baba Halisi akiendelea kuzungumza na Luhanjo wakati wakiagana.
Baba Halisi na Mama Halisi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Luhanjo. Kulia ni Kaka Mnara Mmoja Halisi na Dada Udhihirisho Halisi.
Luhanjo akizungumza na Baba Halisi na Mama Halisi kukamilisha kuagana.
Baba Halisi akiagana na Luhanjo.
Mama Halisi akiagana na Luhanjo.
Luhanjo akiwa ameshaingia katika gari lake kwa ajili ya kuondoka. Kulia ni Amani Halisi wa Kituo cha Arusha.
Baba Halisi na Mama Halisi wakimrakia safari njema, wakati akianza kuondoka.  

Habari/Picha na Msimamizi Mkuu Blog ya Taifa ya CCM, Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages