Baadhi ya wabunge waliokuwa wanasafiri na basi la Shabiby wamepata ajali eneo la Mbande Dodoma, baada ya kugongana na Lori.
Akielezea kwa njia simu kuhusu ajali hiyo, mmoja wa wabunge waliosafiri na moja kati ya mabasi manne ya Shabiby yaliyokuwa yanawasafisha kwenda kwenye mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki Mombasa Kenya, amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri baada ya basi moja kudaiwa kugonga nyuma ya lori lililokuwa limesimama katika Barabara hiyo ya Morogoro - Dodoma.
"Aisee, mambo siyo mazuri, basi moja kati ya manne tuliyokuwa tunasafiria limepata ajali na baadhi ya wenzetu wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali za Uhuru na Benjamini Mkapa kwa ajili ya matibabu, hatujui hadi sasa wenzetu wanaendeleaje, nasi bado tupo eneo la ajali," amesema Mbunge huyo.
Msafara huo ambao ulitakiwa kupitia Chalinze na Tanga kwenda Mombasa, umejumuisha wabunge na watumishi wa Bunge zaidi ya 120 wanaokwenda kushiriki michezo mbalimbali inayotarajia kuanza kesho Desemba 7 hadi Desemba 17 mwaka huu na kushirikisha timu za mabunge ya Nchi 7 likiwemo Bunge la Afrika Mashariki.
Mtandao huu umefanya jitihada za kumtafuta kwa njia ya simu Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP, David Misime amepatikana na kuahidi kuifatilia ajali hiyo na kutoa uthibitisho baadaye.
Tunawaombea majeruhi wa ajali hiyo wapate uponyaji mwema.
CCM Blog ITAWALETEA TAARIFA YA TUKIO HILO KADRI ZITAVYOKUWA ZINAPATIKANA KUTOKA VYANZO HALISI, LIKIWEMO JESHI LA POLISI.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇