LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 10, 2024

CAF YAIONDOA KENYA KUANDAA MICHUANO YA CHAN, YAPEWA RWANDA

 Shirikisho Soka Afrika CAF limetoa taarifa kuwa taifa la Kenya 🇰🇪 limeshindwa kukidhi vigezo vya kuwa mmoja wa mataifa yatakayoandaa mashindano ya CHAN mwakani (2025) baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.


Kwa mujibu wa CAF viwanja vyote vilivyopo Kenya havina ubora wa kutumika katika michezo ya FIFA wala CAF na kwa mujibu wa wakaguzi wa CAF hata Uwanja wa Kasarani unaojengwa pia imeonekana hautakamilika kwa wakati.


 Nafasi hiyo wamepatiwa Rwanda 🇷🇼 baada ya kuonekana wao wamekidhi vigezo vya kuwa wenyeji wa CHAN.


CHAN2025 itachezwa katika mataifa matatu ambayo ni Rwanda 🇷🇼, Tanzania 🇹🇿 na Uganda 🇺🇬.

Uwanja wa Karasani unaoendelea kujengwa.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages