Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu Meja Jenerali Iddi Said Nkambi amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na Kiraia zinazohusika na Ulinzi wa Amani chini ya Mwavuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) kuhakikisha zinandaa mitaala ya kuendeshea mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa kuzingatia matishio yanayozikabili nchi wanachama.
Meja Jenerali Nkambi ameyasema hayo leo tarehe 18 Novemba 2024 wakati wa ufunguzi wa Semina fupi ya siku 5 inayohusu uwasilishaji wa mitaala mipya ya mafunzo itakayotumika kuandaa Majeshi ya SADC, semina inayofanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani (PTC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam.
Semina hiyo inayoendeshwa na Chuo cha Ulinzi wa Amani cha Kikanda chenye Makao Makuu yake nchini Zimbabwe inahudhuriwa na washiriki kutoka nchi wanachama wa SADC ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika kukabiliana na matishio pindi wanapokuwa katika majukumu ya Ulinzi wa Amani ndani ya ukanda wa SADC na sehemu zingine watakapopewa jukumu.
Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu Meja Jenerali Iddi Said Nkambi akiwa katika picha ya pamoja na waliohudhuria mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇