Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Jukumu kubwa ambalo Serikali imekabidhiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2025 kwa kuzingatia maelekezo yote yaliyoainishwa katika kurasa zote zaidi ya 300 za Ilani hiyo, kwa ajili ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua murua katika sekta zote.
Ili kuhakikisha sekta zote, zinasimamiwa kwa ufanisi na kuleta neema kubwa kwa taifa, Ilani hiyo ya CCM imeainisha maelekezo ya kufanywa na serikali ambayo ni kusimamia na muimarisha misingi ya kuziba mianya ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha na umma na kuimarisha uwajibikaji katika sekta zote.
Kwa mfano, katika Ilani hiyo Ibara ya 18 (b) (iv) imeelekeza serikali kuboresha mfumo wa uendeshaji wa Taasisi za Umma na usimamizi wa matumizi ya Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuondoa matumizi yasiyo na tija kwa kwa kuzingatia mfumo wa usimamizi unaofanya kazi kwa ufanisi.
Ili kuzingatia mfumo wa usimamizi unaofanya kazi kwa ufanisi, Ilani hiyo katika sura ya 4 imezungumzia kutumia Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, ikisisitiza kuwa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni nyezo muhimu katika kutatua changamoto hususan katika kuwezesha matumizi ya rasilimali kwa ufanisi zaidi.
Hivyo katika Ibara ya 103, Ilani hiyo ya CCM ikaagiza serikali kuandaa na kutekeleza mikakati ya matumizi ya teknolojia mpya za kidigitali, huku katika Ibara ya 111 ikiagiza Maadili ya viongozi na Watumishi wa umma kuwa suala muhimu na la kipaumbele katika harakati za kujipatia maendeleo.
Kwa ufupi, maelekezo hayo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ndiyo yaliyozaa uwepo Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) baada ya serikali kufanya michakato mbalimbali ikiwemo ya kuundwa sheria iliyoridhia PPRA, na kwa mujibu wa sheria zimeundwa na kukamilika Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 na Miongozo kwa ajili ya kuweka taratibu za ununuzi wa umma.
Jana, Jumatatu, Novemba 4, 2024 PPRA, ilifanya kikao kazi na Wahariri wa Habari kueleza utendaji na mafanikio ya Mamlaka hiyo katika kipindi cha Miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan. Kikao Kazi hicho kiliamdaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao kazi hicho Wazurunguzaji walikuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Dennis Simba na Meneja na Mamlaka hiyo Kanda ya Pwani Vick Mollel, ambao walieleza kwa kina mafanikio ya PPRA, Sheria ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Mfumo wa NeST ulivyoweza kuwa mkombozi katika udhibiti wa ununuzi wa umma ikiwemo Serikali kuongeza bajeti ya ununuzi ya zaidi ya sh. trilioni 38.6 kupitia Mfumo huo.
Kwa kuwa Blog ya Taifa ya CCM (Official CCM Blog) tulikuwepo kwenye Kikao Kazi hicho, tunakuwekea hapa Wasilisho lote kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma Namba 10 ya Mwaka 2023 na Matumizi ya Mfumo wa NeST kama lilivyowasilishwa na PPRA kwenye Kikao kazi hicho.👇
Your Ad Spot
Nov 5, 2024
Home
featured
siasa
ILANI YA CCM ILIVYOIBUA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA NA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST ULIOLETA MAFANIKIO
ILANI YA CCM ILIVYOIBUA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA NA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST ULIOLETA MAFANIKIO
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇