Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (PhD) katika uongozi. Tukio hilo limefanyika leo, tarehe 24 Novemba 2024, wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, katika Kampasi Kuu ya Morogoro.
Heshima hiyo imetolewa kwa kutambua mchango mkubwa wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia katika uongozi, ikiwemo umahiri wake katika nafasi mbalimbali za utumishi ndani ya Chama, Serikali, na hata kimataifa. Mhe. Dkt. Samia pia alihudhuria kama mgeni maalum katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Maekani.
Tukio hili limeonyesha namna mchango wa Rais Samia katika kuimarisha uongozi bora, kukuza maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kidemokrasia, unavyothaminiwa
Rais Samia akionesha tuzo hiyo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi tuzo hiyo Rais Samia.
Rais Samia akiwa na tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇