LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 29, 2024

CCM YATAJA SABABU NNE ZILIZOIVUSHA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, YASEMA CHADEMA WAMEVUNA WALICHOPANDA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Lumumba DSM
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa sababu nne ambazo zimefanya Watanzania kuendelea kukiamini na kuchagua wagombea wake katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kwamba Chadema kubwagwa katika Uchaguzi huo wamevuna walichopanda kwa sababu waliendekeza migogoro na maandamano badala ya kujipanga.


Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi CPA Amoss Makalla, akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kueleza masuala mbalimbali ikiwemo sababu zilizoiwezesha CCM kuibuka na ushindi wa kimbunga katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika juzi, Novemba 27.

Akitaja sababu hizo alisema CCM wanaamini wameaminiwa na wananchi kutokana na sababu mbalimbali ya kwanza ikiwa ni wananchi hao kuridhika na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopo katika mitaa, vitongoni na vijiji na utatuzi wa kero zao mbalimbali. 


CPA Makalla amesema sababu ya pili ni maandalizi bora ya na ya kutosha ambayo CCM ilifanya kuelekea Uchaguzi huo wa serikali za Mitaa kwa kuwa ilijua kutakuwa na huo, hivyo katika maandalizi hayo ilifanya tathimini ya viongozi waliopo katika mitaa, vijiji na vitongoji.

“Kwa hiyo kila eneo kila wilaya tuliwafanyia tathimini viongozi walioko madarakani lakini na kutambua changamoto na maoni ya wananchi. CCM haikukosea kuteua wagombea safi ambao walikubalika na hiyo imekuwa siri ya ushindi lakini pia nyie ni mashuhuda kuanzia ngazi ya kitaifa hadi Mashina, uchaguzi huu tuliuchukulia kwa uzito mkubwa, akasema CPA Makalla.

CPA Makalla, alisema kutokana na hali hiyo hatarajii atokee mtu na kuhoji CCM imeshindaje kwa kuwa hata Watanzania ni mashuhuda kwamba vyama vingine havikuwa na maandalizi, havijaonekana kwa wananchi miezi saba, vingine vimewekeza katika migogoro na maandamano tu.

“Unafanya maandalizi kwa siku tatu unatarajia unaweza kushinda? CCM imefanya maandalizi ya kutosha kupitia viongozi wake. Changamoto ambayo wapinzani wameipata ni kutokana na kutokuwa na maandalizi ya uchaguzi.Tusitafute sababu yoyote". amesema CPA Makalla.

Amesema sababu ya tatu ya ushindi wa CCM ni kwamba imefanya kampeni zake kisayansi kuanzia uzinduzi, kufunga kampeni pamoja uratibu na ushirikishwaji kwa viongozi wa Chama kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina na sababu ya nne ni kuchangiwa vizuri na migogoro ya vyama vya siasa.

"Pamoja na kwamba matatu ya kwanza niliyotaja nzido sababu kuu zilizotufanya kushinda kwa kishindo, lakini migogoro nayo ndani ya vyama vyao imechangia CCM kuibuka na ushindi mnono katika Uchaguzi huo wa serikali za mitaa. Na kwa hili nasema tumefurahi maana adui yako muombee njaa, Chadema Wamevuna walichopanda". akasema CPA Makalla.

Pamoja na kufurahia migogoro kuchangia ushindi wa CCM, lakini CPA Makalaa ametumia nafasi hiyo kuvitshauri vyama vya upinzani kuendelea kuvumiliana na kujiepusha na migogoro kwa kuwa chama chenye migogoro ni vigumu kushinda katika uchaguzi, akitolea mfano wa Chadema ambao alisema kwa sasa wana mgogoro mkubwa na kwamba imeshuhudiwa Arusha wanachama wakivurugana na kupigana wakati wakielekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

“Najua vyama vya upinzani leo vinaongea lakini watakachoweza ni kutoa propaganda tu kwa kuituhumu TAMISEMI na CCM lakini ukweli wameshindwa uchaguzi kwasababu ya kutokuwa na maandalizi na migogoro kwa viongozi wao. Mengine yote watakayosema hayana ukweli.” akabainisha CPA Makalla.

CPA Ammos Makalla akizungumza na Waandishi wa habari, leo CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages