LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 20, 2024

CCM YAAGIZA BATI MBOVU ZING'0LEWE HOSPITALI YA PANGANI

 Uongozi wa Wilaya ya Pangani umeagizwa bati zote zisizo kidhi viwango vya ubora kutoka Shirika la  Viwango Tanzania (TBS) na kuezekwa katika hospitali ya Wilaya hiyo, ziondolewe, ziezekwe bati mpya.


Aidha, wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuwa waaminifu katika usambazaji wa vifaa vya ujenzi kwenye miradi ya Serikali ili kuepuka ubora duni wa vifaa katika miradi muhimu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdurahman Abdallah, alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la hospitali kongwe ya Wilaya ya Pangani, uliopewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

Katika ziara hiyo, Abdallah alisisitiza kuwa ni jukumu la CCM, yenye Ilani inayotekelezwa, kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi inayopokea fedha za Serikali ili kuhakikisha rasilimali hizo zinatumika ipasavyo.

“Kama Chama, ni wajibu wetu kuhakikisha fedha zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika kama ilivyokusudiwa, hivyo, tunatembelea miradi ili kujionea maendeleo yake,” alisema  Abdallah.

Akizungumzia suala la bati zilizokosa ubora katika hospitali hiyo,  Abdallah alisema kuwa waligundua tatizo hilo na kutoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya kuhakikisha bati hizo zinabadilishwa mara moja ili kuzingatia viwango vya TBS.

"Mimi nasisitiza tena, ni lazima bati hizi zote ziondolewe na ziezekwe bati zinazokidhi viwango ili kuhakikisha mradi huu unaendelea kwa ubora na manufaa kwa wananchi," alisema.

Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdurahman Abdallah akitoa agizo hilo alipotembelea hospitali hiyo.
Jengo la hospitali ya Pangani ambayo jengo lake limeezekwa kwa bati zisizo na ubora.
Abdallah akizungumza na mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo.


Abdallah akitembelea hospitali hiyo.
Abdallah aakiwa na viongozi wengine wakiangalia gari la kubebea wagonjwa katika hospitali hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages