LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 19, 2024

TUME YAWAPIGA MSASA MAOFISA WA POLISI KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Maafisa wa Polisi nchini wametakiwa kujenga  tabia ya kujikumbusha sheria mbalimbali ikiwemo zinazohusu masuala ya uchaguzi ili kuepuka kuyumbishwa na
wanasiasa wanaoamua kupotosha yaliyomo katika sheria hizo kwa maslahi yao binafsi.Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani wakati akifungua mafunzo ya Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini yaliyofanyika
 Oktoba 17, 2024 mkoani Dodoma.

Kailima amesema, mafunzo ya aina hii ni
muhimu kwa kipindi hiki ambacho kuna Sheria Mpya mbili zinazosimamia masuala ya
Uchaguzi. Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024
na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024.

“Katika sheria zote mbili yapo mabadiliko
makubwa katika maeneo mbalimbali ambayo ni muhimu sana kwenu kuyafahamu kipindi
hiki ambacho uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga unaendelea na mwakani
itakuwa ni uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisema Kailima.

Aliongeza, mafunzo hayo kuhusu sheria za
uchaguzi yana umuhimu na maana kubwa katika maandalizi ya zoezi zima na
mchakato wa kuelekea chaguzi zilizopo mbele yetu kama Taifa.

“Uelewa wenu kuhusu sheria hizi, utasaidia
sana usimamiaji wa sheria na kuchukua hatua za udhibiti wa uvunjifu wa sheria
hizo pamoja na sheria zingine ili watakaokiuka sheria hizo waweze kufunguliwa
mashtaka ipasavyo na kuwatendea haki kwa kitakachoamuliwa na Mahakama,”
alisisitiza Kailima.

Aliendelea kwa kusema kuwa, anaamini kuwa
baada ya mada inayohusu sheria za uchaguzi kuwasilishwa wakuu hao wa upepelezi
watakuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kwenda kuboresha taarifa zao katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pindi zoezi linapofanyika katika maeneo yao.

Lengo la mafunzo kwa maafisa hayo ni
kuwajengea uelewa kuhusu haki za vyama, wananchi na makundi mengine katika
vipindi vyote vya uchaguzi, kwa maana kabla ya uchaguzi Mkuu, wakati wa
uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Pamoja na masuala ya Sheria za uchaguzi, washiriki
hao ambao ni Wakuu wa Upelelezi walipata kujua wajibu wa Jeshi la Polisi wakati

wa uchaguzi, Bank Note Security features, utambuzi wa bidhaa bandia na hatimiliki,
upelelezi sambamba na utafiti katika mapungufu ya kisheria.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa

ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya siku
moja kuhusu sharia za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma. Pamoja nae ni Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai. 
                                        

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai (kulia) akifafanua jambo  akati wa mafunzo ya siku moja kuhusu sharia za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani.

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Selemani Mtibora akiwapitisha katika maeneo muhimu yaliyomo kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya
mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024.

Mkurugenzi wa Daftari na Tehama wa INEC, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai wakati wa mafunzo ya siku
moja kuhusu sheria za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma. 

 

Washiriki wakifuatilia mada 

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages