LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 13, 2024

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wananchi wa Sengerema na Misungwi Mkoani Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mama mzazi wa mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) mara baada ya kuwasili Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la JP. Magufuli lenye urefu wa km 3 pamoja na barabara za maungio zenye urefu wa km 1.66. Mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024. Daraja hilo limefikia asilimia 93 za ujenzi na linatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2025.


Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Sengerema mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.


Muonekano wa Daraja la JP. Magufuli linalounganisha eneo la Kigongo (Misungwi) na Busisi (Sengerema) lenye urefu wa km 3 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66. Mkoani Mwanza tarehen 13 Oktoba, 2024. Ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 93 na linatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2025.( PICHA NA IKULU)

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages