LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 22, 2024

CCM YAFURAHISHWA UANDIKISHAJI WANANCHI DAFTARI LA WAPIGAKURA KUGONGA ASILIMIA 96.7 DAR

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimefurahishwa na mwikitkio wa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapigakura kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taiafa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenrzi, CPA Amos Makalla akipokea taarifa ya uandikishaji wananchi katika daftari la mkaazi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam, ilipowadilishwa kwake na viongozi wa Chama mkoa huo, leo Oktoba 22, 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Nianze kwa kuwapongeza Viongozi wa CCM ngazi zote tangu mkoa hadi Mabalozi, Wafuasi wa CCM na Wananchi kwa jumla, yaani mkoa mzima wa Dar es Salam kwa kutoa ushirikiano katika kazi ya Uandikishaji hadi kufikia asilimia 96.7, hii ni faraja kwa CCM, kwa kuwa Dar es Salam ni uso wa Nchi.

Awamu hii Wananchi wamejiandikisha kwa wingi sana na hii imechagizwa na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM hilo halina kificho kwa sababu miradi haitekelezwi hewani,Miradi ya Zahanati, Madarasa,Vituo vya Afya imetekelezwa kwenye Vijiji na Vitongoji hivyo Wananchi wameona kazi ya Dk. Samia Suluhu Hassan.

CPA Makalla amesema endapo chama hicho tawala hapa nchini kitapoteza kwenye baadhi ya vitongoji, vijiji au mitaa vitaheshimu matokeo hayo na kwamba huo utakuwa wakati muafaka kwao kujitafakari na kujipanga kwa nini walipoteza eneo hilo, ili uwe njia ya kufanya vizuri kwenye uchaguzi ujao

Amesema taarifa iliyotangazwa na Waziri wa Tamisemi hakushangaa kwani takwimu ndani ya Chama zinaonyesha kumekuwa na muitikio mkubwa ni kwa sababu ya kukubalika kwa CCM hasa utekelezaji wa Ilani mzuri ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi hilo halina kificho na Watanzania wanaona .

"Miradi hii haitekelezwi hewani, miradi hii ya Zahanati, madarasa, vituo vya afya inatekelezwa katika maeneo ya vitongoji, vijiji na mitaa kwa hiyo wananchi wa Tanzania wanaona hivi vitu, wanaona namna ambavyo Rais Samia (Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa) amevunja rekodi ya kupeleka fedha za maendeleo katika kila eneo, na kwa maana hiyo wamevutiwa sasa kuona wanaweza wakawasimamia viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaopelekewa fedha hizo ili kuona maendeleo yanaendelea kuwepo kwenye vijiji na mitaa yao ndio maana kuwekuwa na muamko huu" -Makalla

Akizungumzia kuhusu hamasa ya Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Daftari la Mpiga kura- amesema
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia amekuwa chachu kubwa kwa Wananchi wengi kujiandikisha kwa sababu Wananchi wengi walipata ishara kuwa Uchaguzi ni muhimu kwani wengi waliona kama Rais amejitokeza na huyu ndie anaepeleka pesa mpaka ngazi ya kijiji wengi wakajitokeza amekuwa Kiongozi wa mfano lakini upande wa pili hawakufanya hivyo.

CCM Dk. Samia amejiandikisha ,Balozi Nchimbi amejiandikisha,Wa NEC , Viongozi wote wa Jumuiya na Mikoa mpaka Wilaya wamejiandikisha 

"Wananchi walipomuona Dkt Samia anaenda Kujiandikisha pamoja Viongozi wakuu wa Chama na Serikali kuanzia ngazi za Mikoa mpaka Wilaya kila eneo hilo tu lilitosha kuleta hamasa kwamba Uchaguzi huu ni muhimu na mana wakajitokeza" CPA Makalla

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa Vyombo vya habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages