LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 9, 2024

YAHYA MSANGI: IPO SIKU MUUMBA ATAMUUMBUA 'MASTERMIND' WA UTEKAJI NA MAUAJI.

"Sasa kila ukisoma post utaona watu wakisikitika kifo cha mwenzetu, Kada na Kiongozi wa Chadema. 


Marehemu ni mtu ambaye tulikuwa tukitaniana sana hasa X na Facebook, akipenda sana kuniita nimtanie au nimsome Chicco Paris . 


Japo hatukuwa chama kimoja lakini tukitaniana na kukosoana kwa heshima, marehemu hakuwa mtukanaji kama wenzake, alikuwa na maadili mema. Allah amfanyie wepesi inshallah.


Lakini ukiwasoma Chadema na viongozi wao tayari wanamhukumu kuwa kauawa na serikali. Hapo ndipo nimeona nijaribu kuhoji haya:


1. Inawezekanaje mtu ajue mwingine alivyotekwa ndani ya basi na baada ya saa 12 mtu huyohuyo ajue kafa na aelezee mwili ulivyo? Alipataje hizi taarifa?


2. Hivi marehemu alikuwa na tishio gani kubwa hadi serikali iamue imuue? Hivi kati ya marehemu na Karo, Lissu na Mbowe nani walau unaweza kusema anaisumbua serikali? Kwa Nini wao serikali haiwaui? 


3. Inawezekana vipi aliyetangaza kutekwa na kuuawa anakuwa wa kwanza kufika mochwari kabla hata ya ndugu wa marehemu na kudai atasimamia post mortem? 


4. Mtu tuliyesikia yuko kambi ya Lissu na anahoji nafasi ya Mwenyekiti na matumizi na akitangaza nia kugombea nafasi mojawapo inaonekanaje anapofikwa na umauti hivi? Mbona kama Chacha Wangwe?


5. Kwa nini visa hivi havitokei kwa ACT, NCCR au TLP? Kuna chama kikuu cha upinzani kuzidi ACT? Kwa vigezo vyote hakuna chama tishio kwa CCM kuizidi ACT.  


ACT ndicho kimefanikiwa kushika "robo mkate" kule Zanzibar. Ndicho kinahodhi karibu Pemba yote. Ndicho chenye wabunge wengi Baraza la Mapinduzi na Bunge la JMT. Kama kuuawa basi ingekuwa wao na si CHADEMA ambacho hakina nguvu yoyote zaidi ya mikwara😀


Tunaomba vyombo vya dola vitumie kifo hiki kuwapatia watanzania ukweli. Mpanga utekaji na mauaji yupo".



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages