Na Oscar Assenga, TANGA.
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amesema kwamba mkoa huo
umejiandaa kikamilifu kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku
akiwaonya watu wenye tabia ya kung’oa orodha ya wapiga kura wasisubutu
kufanya hivyo.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 27
mwaka huu ambapo alisema watakaojaribu kufanya hivyo hawatasalimika
badala yake watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo faini ya Laki
tatu,kifungo cha miezi 12 au vyote vya pamoja
Balozi Batilda
aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea
maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa huo ambapo
alisema hawataki kuona vitendo hivyo vinatokea kwenye mkoa huo.
Alisema
kwa sababu orodha hiyo imewekwa maalumu kwa ajili ya kuwawezesha wapiga
kura wa eneo Fulani kuweza kuhakiki majina yao ili waweze kushiriki
kwenye uchaguzi huo hivyo wanapotokea watu wanang’oa ni uvunjifu wa
sheria.
“Lakini pia kutoa taarifa za uongo ili uweze kugombea
nafasi ya za uongozi pamoja na wale ambao watajiandikisha zaidi ya mara
moja anatoka sehemu moja hadi nyengine hao nao wakibainika watachukuliwa
hatua kali”Alisema
Aidha alisema kwamba pia wale ambao
watabainika wamepiga kura zaidi ya mara moja au kutishia wapiga kura ni
kosa na watachukuliwa hatua za kisheria sambamba na wale ambao watafanya
kampeni wakati wa uchaguzi.
“Lakini kwa wale ambao wataonyesha
ishara au kuvaa mavazi yanayomuashiria mgombea hayo mabango yakionekana
wakati wa uchaguzi ni kosa na watakaobainika watashughulikiwa”Alisema
Onyo
hilo pia alilitoa kwa wale wenye tabia ya kuwazuia wasimamizi wa
Uchaguzi kutekeleza majukumu yao wakati wa zoezi la watachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Kuhusu ukomo wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Alisema
kwamba viongozi hao ukomo wao utakuwa ni Octoba 25 mwaka huu kwa
viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji na siku saba za ukaguzi na
kuanzia Octoba 1 mpaka 7 utakuwa ni muda wa kuchukua fomu na kurudisha
na Octoba 8 na 9 utakuwa uwasilishaji pingamizi kuhusu uteuzi na kuanzia
Octoba 20-26 itakuwa ni kipindi cha kampeni.
“Kwa mkoa wa Tanga
tunatarajia kuwaandikisha wapiga kura wasiopungua chini ya asilimia 80
na kuendelea kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Hata
hivyo alisema nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo hutegemea aina
ya Halmashauri inayofanya uchaguzi kama ni Mamlaka ya Wilaya au Mji kwa
upande wa mkoa wa Tanga wana maeneo ya utawala yanayohusika kwenye
uchaguzi ni mamlaka ya mji mdogo ni tatu,Kata 245,mitaa 270,vijiji 763
na Vitongoji 4,531.
Your Ad Spot
Sep 17, 2024
RC BATILDA AWAONYA WATAKAONG’OA ORODHA YA WAPIGA KURA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇