LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 8, 2024

RAIS DK. SAMIA ATEUA WAKURUNZI WAKUU MAMLAKA ZA USAFIRI WA ANGA NA VIWANJA VYA NDEGE

Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan amemteua Salim Ramadhani Msangi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo Semtemba 8, 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka imesema, pia Rais amemteua Abdul Athumani Mombokaleo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

''Kabla ya uteuzi huo Mombokaleo alikuwa Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), amechukua nafasi ya Mussa Mbura ambaye atapangiwa kazi nyingine", Taarifa hiyo imesema.

Rais Dk. Samia akiwa kazini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages