Shirika la Omuka Hub lililo chini ya Mhe Neema Lugangira ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Madereva wa Pikipiki na Wamiliki kwa Bukoba Mjini wamezindua Kozi Namba 1 ya Usalama Barabarani ambapo Bodaboda 180 watapata mafunzo ya udereva na cheti bure ili waweze kupata leseni na gharama zote zimelipiwa na Omuka Hub ambayo pia itachangia nusu ya gharama ya leseni.
Dhamira ya Omuka Hub ni kuwafikia wanachama wote katika Chama Cha Madereva wa Pikipiki na Wamiliki kwa Bukoba Mjini awamu moja baada ya nyingine kwa lengo la kuimarisha usalama barabarani, kupunguza ajali, kuokoa maisha pamoja na kuwaunganisha vijana wetu na fursa mbalimbali.
Aidha, katika Uzinduzi, Vijana wa Bodaboda walipokea elimu kuhusu fursa za kujiunga na NSSF na walianza kujisajili.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Kozi Namba 1 ya Bodaboda alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera (RPC) ACP Yusuph Daniel.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇