LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 9, 2024

DK. DIMWA: WATAKAOHAMIA CCM TUTAWAPA FURSA NA HAKI SAWA NA WANACHAMA WENGINE

Na Is-haka Omar, Zanzibar
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amesema Chama  kipo tayati wakati wowote kuwapokea  wananchi mbalimbali wanaotoka katika vyama vya upinzani na kuhakikisha wanapata haki na fursa sawa kama walivyo Wanachama wengine ndani ya chama.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiwapokea Wanachama wapya zaidi 90 kutoka ACT-Wazalendo katika Shehia ya Wingwi Mapofu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika mwendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,CCM Taifa Zanzibar.

Dkt.Dimwa,ameeleza kwa milango ya CCM ipo wazi kwa Wananchi wa makundi mbalimba kujiunga na Chama hicho ili wanufaike na siasa imara zinazojali utu,usawa,haki na demokrasia yenye tija kwa wote.

Alisema Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi,imetekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa zaidi ya asilimia 90 katika kuimarisha sekta za Elimu,maji safi na salama,afya,kilimo,uvuvi,ujenzi wa maeneo huru ya uwekezaji na viwanja,ujenzi wa Bandari za kisasa za Shumba na Wete,barabara za kisasa ndani ya Mkoa huo.

Alisema zawadi pekee ya kuunga mkono juhudi hizo za Dk. Mwinyi ni Wananchi bila kujali tofauti za kisiasa, kidini na kikabila kuhakikisha wanawapigia kura nyingi za ndio wagombea wote wa CCM katika uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka 2025.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa,alisema lengo la ziara hiyo ya kikazi ni kuimarisha Chama Cha mapinduzi na jumuiya zake,kuwakumbusha Wanachama,Viongozi na watendaji wake kujiandaa na uchaguzi mkuu wa dola ujao.

Alitoa wito kwa Wanachama wote waliotimiza umri wa miaka 18 kuhakikisha wanajiandikisha katika awamu ya pili ya zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate uhalali wa kupiga kura.

Alisisitiza kuwa Chama Cha mapinduzi kimejipanga vizuri katika uchaguzi mkuu ujao na kitashinda kwa kura nyingi zaidi ya asilimia 80,ushindi utakaobadili historia ya siasa ya Zanzibar toka kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

"Chama Cha Mapinduzi kimetokana na wakwezi,wakulima na wafanyakazi hivyo asili yake ni Chama halisi kilichotokana na waafrika wenyewe waliofanya mapinduzi kwa ajili ya ukombozi wa Wananchi na kwa sasa tunaendelea kufanya Mapinduzi ya kiuchumi na maendeleo ili sote tunufaike na matunda ya waasisi wetu.

Tunaendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo ili sekta zote za kiuchumi na kijamii zitoe huduma Bora inayokidhi mahitaji ya Wananchi wote wa Mjini na vijijini."alisema Dkt.Dimwa.

Aliwataka Wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kupuuz propaganda na siasa za uchochezi zinazifanywa na vyama vya upinzani nchini hasa Chama Cha ACT-Wazalendo na badala yake wapime mafanikio ya sera za CCM na ACT&Wazalendo kisha wafanye maamuzi sahihi ya kuchagua chama kinachofaa kuongoza dola.

Alitumia ziara hiyo wambia Wananchi kuwa hakuna chama chochote cha upinzani nchini chenye hati miliki ya kisiwa cha Pemba hivyo kila chama Cha kisiasa kina haki ya kunadi sera ili zikubalike kwa Wananchi na kiongoze dola na sio kufanya siasa za ubabe na fitna dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa,alisema Mkoa huo unaendelea kutekeleza kwa vitendo kazi za chama Cha mapinduzi na kuisimamia Serikali itekeleze vizuri Ilani ili Wananchi wapete huduma Bora.

Akizungumza kwa niaba ya Wanachama waliotoka ACT-Wazalendo na kujiunga na CCM Khamis Juma Hamad, Shehia ya Wingwi Mapofu Jimbo la Micheweni,alisema sababu ya kujiunga na CCM nikutokana na kupewa ahadi hewa na kutumia kwa maslahi binafsi ya Viongozi wa ACT-Wazalendo na wanapopata matatizo wanatelekezwa.

 "Wananchi wa Kaskazini Pemba kwa sasa tumeamka na kufuata Chama cha Mapinduzi chenye Viongozi wakweli na wangwana wanaojali maslahi ya makundi yote hivyo sisi wenye tumejiunga kwa hiari yetu kuunga mkono Dk.Mwinyi na wapo wengi wanakuja kutoka ACT-Wazalendo jiandaeni kuwapokea."alisema Hamad.

Alieleza sera za Chama Cha Mapinduzi zimekuwa ni mkombozi kwa wananchi wa Kisiwa cha Pemba kwani wananufaika na maendeleo katika nyanja mbalimbali bila kubaguliwa kwani watoto wao wanasoma katika skuli za ghorofa bila kujali tabaka la kipato,barabara kuu na za ndani zimejengwa kwa rami pamoja na kujengewa hosptali za kisasa mijini na vijini.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapunduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akipokea kadi za waliokuwa wanachama wa ACT-Wazalendo 90 wakajiunga na CCM katika Jimbo Wingi Shehia ya Wingwi Mapofu.
 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapunduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akipandisha Bendera ya CCM katika Maskani ya waliokuwa wanachama wa  ACT-Wazalendo waliojiunga na CCM katika Jimbo la Wingwi shehia ya Wingwi Mapofu Wilaya ya Micheweni.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapunduzi(CCM) Zanzibar Dkt. Mohamed Said Dimwa, akizungumza na sheha mstaafu wa shehia ya Micheweni ndugu Dawa Juma Mshindo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages