Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, kimetamba kitajizolea viti katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024, kutokana na kiwango kikubwa ilichofanya katika utekelezaji wa Ilani, katika Kata zote wilayani humo.
Tambo hiyo imesemwa na Kamisaa wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya hiyo kupokea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/ 25, katika kipindi cha miaka minne kuanzia 2020/21 na 2023/24, kilichofanyika leo Septemba 6, 2024, katika Ukumbi wa Soko la Magomeni.
"Kwa kweli tumshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha nyingi ambazo zimetuwezesha kutekeleza ilani ya Uchaguzi kwa ufanisi mkubwa katika sekta zote, ikiwemo afya, elimu na huduma nyingine za jamii. Sasa kwa namna tulivyotekeleza ilani hakuna sababu ya kukosa kiti hata kimoja katika Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu.
Tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kila mmoja wetu tangu Wana CCM na watendaji wa serikali tunakwenda kwa wananchi kueleza mambo mbalimbali tuliyotekeleza ili wayajue kinagaubaga. Tukifanya hivyo kwa bidii hakuna shaka ya CCM kujizolea viti vyote", alisema DC Mtambule na kuongeza;
"Mnajua mkikaa tu mkidhani wananchi wote wanayajua yaliyofanyika na tunayoendelea kuyafanya inakuwa siyo sawa, maana tazama kwa mfano Halmashauri yetu ya Manispaa, imevuka kiwango cha ukusanyaji mapato, lakini hata humu ndani wamo wana CCM ambao hata hawajui".
Akieleza hoja zilizotolewa na Wajumbe katika Kikao Cha Halmashauri kilichofanyika Mei 7, mwaka huu, DC Mtambule alisema, Serikali ya Wilaya imeyafuatilia yote na mengi yamepatiwa ufumbuzi, ikiwemo suala la Wakandarasi wa kuzoa taka ambao baadhi walisemwa kuwa hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
DC Mtambule alisema, katika kushughulikia suala hilo Mkurugenzi wa Halmashauri alifanya mabadiliko ya wakandarasi hao na wengine kupunguza maeneo wanayoshughulia hasa katika maeneo ya Makumbusho na Mikocheni, hata hivyo akasisitiza kwamba suala la usafi ni endelevu hivyo ni lazima kukabiliana nalo kwa juhudi zote kuhakikisha uchafu siyo rafiki, ili usichafue sura nzuri ya manispaa.
Kuhsu changamoto ya barabara DC Mtambule alisema, kwa kushirikiana na serikali Kuu na Manispaa Uongozi wa Wilaya umeshughulia maeneo mengi, lakini akakiri changamoto bado ipo katika maeneo mbalimbali lakini wataendelea kuikabili hatua kwa hatua.
"Katika Manispaa yetu tuna kilometa 1658 lakini katika hizo 250 ndiyo za lami, nyongine zote ni za udongo na za changarawe hivyo hizi za udongo na changarawe huhitaji ukarabati wa mara kwa mara. Tunaishukuru Serikali kupitia TARURA imekuwa ikizifanyika ukarabati barabara hizi na kwa sasa nyingi zinapitika.
Tuanchofanya kwa sasa ni kuhakikisha zile barabara ambazo ni mbovu zaidi tunazifanyika ukarabati ili walau ziweze kupitika. kuna badabara kama ile ya Mbopo, ile ambayo iliharibika baada ya daraja kuzolewa na mafuriko, ile sasa itatengenezwa tena kwa lami ili iweze kupitika", alisema DC Mtambule.
Badaye DC Mtambule alieleza kwa muktasari yaliyoandikwa katika Kitabu chenye kurasa 412 kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mnne kuanzia mwaka wa fedha wa 2020/21 hadi 23/24 na baadaye kutoa fursa kwa wajumbe kujadili.
Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa ni Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati za Mitaa na fomu za wagombea wa nafasi hizo ambao ni kutoka vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu zitaanza kutolewa Novemba Mosi hadi 07, 2024 na kampeni za uchaguzi zitaanza Novemba 20 hadi 26,2024.Kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/
25, kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2020/21 na 2023/24, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya
CCM Wilaya hiyo,
kilichofanyika leo Septemba 6, 2024, katika Ukumbi wa Soko la Magomeni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kinondoni Abdallah Shaweji.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Abdallah Shaweji akizungumza katika Kikao hicho.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinodoni Jacob Siai akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Ibrahim Msengi akizungumza jambo na Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Dar es Salaam Ally Bananga wakati wa kikao hicho.
Viongozi meza Kuu wakiwa wamesimama wakati DC Mtabule (kulia) akiimbisha wimbo 'tuna imani na Samia (Rais Dk. Samia)' baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM wiayani humo.
Wajumbea wakishiriki kuimba wimbo huo.
Wajumbea wakishiriki kuimba wimbo huoViongozi meza kuu wakishiriki kuimba wimbo huoWajumbe wakiwa wameketi kuendelea na kikao hicho.
Katibu Siai alipokuwa akizungumza mwanzoni mwa kikao hicho.
MNEC Msengi alipokuwa akizungumza mwanzoni mwa kikao hicho.
Mwenezi Bananga alipokuwa akizungumza mwanzoni mwa kikao hicho.
Baadhi ya watendaji wa sekta mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa wameketi kuendelea na kikao hicho.Wajumbe wakiwa wameketi kuendelea na kikao hicho.Wajumbe wakiwa wameketi kuendelea na kikao hicho.
Your Ad Spot
Sep 6, 2024
Home
featured
siasa
CCM KINONDONI YATAMBA ITAZOA VITI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KWA KUBEBWA NA UTEKELEZAJI MAHIRI WA ILANI
CCM KINONDONI YATAMBA ITAZOA VITI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KWA KUBEBWA NA UTEKELEZAJI MAHIRI WA ILANI
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇