Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameupongeza uongozi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kujenga jengo zuri la kisasa kwa gharama nafuu ya sh bilioni 9 badala ya sh Bilioni 13 zilizotengwa awali kwa ajili ya ujenzi huo uliochukua miezi 18 kukamilika katika eneo la Medeli jijini Dodoma.
Aidha, ameuagiza uongozi huo kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi zinazoendana na uzuri wa jengo hilo.
Ameyasema hayo alipkuwa akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo hilo Septemba 13, 2024.
Dk. Biteko akihutubia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mramba akizungumza wakati wa hafla hiyo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇