DODOMA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imeweka mipango na mikakati ya kuhakikisha
watoto wanapata malezi bora yanayolenga kukuza ustawi wao.
Mhe.
Ridhiwani amebainisha hayo Agosti 16, 2024 wakati wa makabidhiano ya vyerehani
vya mafunzo ya vitendo kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya
kulelea Watoto Kikombo, Jijini Dodoma.
Aidha,
amesema kuwa dhamira ya serikali inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu
Hassan ni kuboresha ustawi na malezi ya watoto nchini ambao ni vijana na
wataalamu wa baadae.
Vile
vile, Mhe. Ridhiwani ametaka Wizara,
Walezi na Idara zinazohusika kuwashirikisha wadau wa maendeleo ya Jamii ili
kuhakikisha vituo vya kulelea watoto vinafanana katika kutoa huduma bora.
Awali
akizungumza, Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalumu, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na
serikali katika huduma za ulinzi na usalama wa watoto zinazotolewa katika kituo
hicho kwa maslahi mapana ya Taifa.
Naye,
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Zuhura Yunus amesem ugawaji wa vyerehani hivyo ni hatua nzuri kwa WCF kutambua
umuhimu wa kundi hilo kupata ujuzi.
Naye,
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma amesema vyerehani ambavyo vimekabidhiwa
katika kituo hicho ni utekelezaji wa sera ya kurejesha kwa jamii na miongoni
mwa walengwa ni makundi maalum wakiwemo watoto hao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇