LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 16, 2024

MANISPAA YA K'NDONI YAPAZA KILIO AGIZO LA KUSITISHWA UJENZI WA SHULE MTAA WA PANGA, WASHAURI SERIKALI ILITAFAKARI KWA KINA, WASEMA MKASA UNA HARUFU YA UPINZANI

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM

Madiwani Manispaa ya Kinondoni wakiongozwa na Meya Songoro Mnyonge wamepaza kilio chao kufuatia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro kuagiza kusitishwa ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la mtaa wa Panga, Tegeta Wazo Jijjini Dar es Salaam, hivi karibuni.


Madiwani na Meya huyo walipaza kilio hicho, mwishoni mwa Kikao cha kawaida cha robo ya nne ya Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 16, 2024.


"Waheshimiwa Madiwani, juzi juzi Agosti 12, 2024 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro alitoa amri ujenzi wa shule tuliokuwa tumeuanza pale mtaa wa Panga, Tegeta katika Kata ya Wazo usimame, akisema ni Uwanja wa michezo.


Simpingi mheshimiwa waziri lakini naomba serikali iitafakari vizuri hatua hiyo, maana kiukweli waliomlalakia Waziri siyo Wananchi hasa kama wananchi bali ni kundi la wapinga maendeleo yanayofanyika hasa kuelekea nyakati hizi za uchaguzi, kwa hiyo jambo lina harufu ya kisiasa, wanataka kutukwamisha ili serikali inayoongozwa na CCM ionekane hajafanya kitu", akasema Meya Songoro.


Meya Songoro alisema, hatua ya Manispaa ya Kinondoni kujenga shule hiyo ilitokana na ombi la wananchi kindakindaki kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hasan, kuomba wajengewe shule ili watoto wao waachane na adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shule.


"Wakati Rais wetu mpendwa Dk. Samia alipokuwa akienda kufanya filamu ya Tanzania Royal Tour aliamua kusimama pale Tegeta akawauliza Wananchi kero kubwa inayowakabili na sisi tukiwepo, wananchi walimwambia wanahitaji kujengewa shule ya msingi kwa sababu watoto wao wanasumbuka kwenda kusoma shule zilizopo mbali.


Katika kukidhi kiu yao Rais alitoa sh. 433 ili kujengwa shule hiyo. Wananchi walifurahi hata wakaadi shule ikijengwa iitwe shule ya msingi Samia", Akasema Meya Songoro Mnyonge.


Alisema, kwa kuwa wananchi walitoa ombi uongozi wa Manispaa tukiwa pale tukaamua kulifanyia kazi haraka.


Alisema, ili kuhakikisha ujenzi utoe shule yenye hadhi kulingana na jina la Rais, mbali na fedha (sh. Milioni 433) za Rais Samia, katika bajeti ya mwaka huu Manispaa imeongeza zaidi ya Sh. Milioni tisa kufanyika ujenzi wa shule hiyo na kwamba hadi sasa Manispaa imeshaingia gharama ya zaidi ya sh. Milioni 60 ambazo ni sawa na ujenzi wa vyumba vitatu vya madasa.


"Kwa kuwa tuliona pale ni padogo kuweza kujenga shule kubwa yenye hadhi, tuliamua tujenge jengo la orofa nane, ambalo lingekuwa na vyumba 18 vya madasa na vyoo 33, kwa kweli ingekuwa shule ya kisasa kabisa", alisema Meya.


Alisema, uamuzi uliofanywa na Waziri huenda ulighubikwa na jazba hivyo ipo haja ya kuutafakari upya.


"Nashauri, uamuzi huu ufanyiwe tafakuri ya kutosha, Waziri Dk. Ndumbalo akae na Waziri wa elimu, ili jambo hili walitafari kwa pamoja, maana michezo na elimu vyote ni muhimu lakini elimu ni muhimu zaidi kwa sababu ndiyo inayisaidia hata kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.


Kama ni Uwanja wa michezo, katika eneo lile upo uwanja unaomilikiwa na Kanisa moja, ule tunaweza kuzungumza nao ukatumiwa pia na vijana kufanya michezo na hata ikibidi kuuboresha kunaweza kuuboresha", akasema Meya.


Katika hatua nyingine Meya alisema baada ya agizo la Waziri Dk. Ndumbalo la vifaa vyote viondolewe na uwanja kurejeshwa hali ilivyokuwa, wezi wameanza kuiba vifaa mbalimbali zikiwemo nondo.

Katika kikao hicho, Madiwani walisomewa na kuthibitisha muhtasari wa Baraza lao la Juni 10, 2024, Kuthibitisha taarifa ya utekekezaji kazi za Kamati za kufumu za Halmashauri na Taarifa ya Mkurugenzi (utejelezaji wa miradi ya naendeleo) robo ya nne ya kipindi cha Aprili-Juni 2024.


Akisoma taarifa ya Kamati ya Fedha na Uchumi, Mwenyeki wa Kamati hiyo Meya Songoro alisema kwenye wigo huo Manispaa 'imeupiga mwingi'.


"Kipindi hiki tumevuka lengo la makusanyo hadi kufikia asilimia 102 tofauti na kipindi kilichopita cha mwaka jana ambacho tulifikisha asilimia 96.


Sasa fedha tumevuka nazo hivyo matarajio yetu utekekezaji miradi katika kata zetu 20 utaenda vizuri wanaotarajia mkono utakatika, hautakatika, mambo kuchere", alisema Meya.


Alisema, mambo yameenda vizuri kutokana na mifumo iliyotumika kudhibiti uvujaji mapato ikiwemo mifumo ya Tausi iliyosaidia kufanya makusanyo mengi.


Aliwataka madiwani kusimamia ili kuhakikisha vituo vya ukusanyaji kodi vinaimarishwa ili walipakodi walipie huko waliko badala ya kulazimika kwenda kulipia Manispaa.

HABARI KATIKA PICHA

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akizungumzia sakata la Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro kuagiza kusitishwa ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la michezo lililopo mtaa wa Panga, Tegeta Wazo Jijjini Dar es Salaam, hivi karibuni. Meya amezungumza hayo wakati akihitimisha Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani robo ya nne, katika ukumbi wa Manispaa hiyo, leo Ijumaa, Agosti 16, 2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hadija Hamza.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akienda ukumbini kuongoza Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani robo ya nne, katika ukumbi wa Manispaa hiyo, leo Ijumaa, Agosti 16, 2024.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akiongoza kuimbwa wimbo wa taifa, mwanzoni mwa Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani robo ya nne, katika ukumbi wa Manispaa hiyo, leo Ijumaa, Agosti 16, 2024.
Madiwani wakishiriki kuimba wimbo wa taifa..
Maafisa mbalimbali na waalikwa kutoka taasisi
wakishiriki kuimba wimbo wa taifa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akiongoza dua, mwanzoni mwa Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani robo ya nne, katika ukumbi wa Manispaa hiyo, leo Ijumaa, Agosti 16, 2024.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hadija Hamza, akisoma ajenda za kikao na kumkaribisha Meya kuongoza kikao.
Meya akigungua kikao.
Meya akimkaribisha mdau kutoka Benki ya DCB kuzungumza,
Mkurugenzo Mtendaji wa Benki ya CDB Sabasaba Moshinsi akizungumza.
Masiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Wahusika mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Wahusika mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho. Kisha Wenyviti wa Kamati mbalimbali wakatoa hoja na mapendekezo ya kamati zao.👇
Mwenyekiti kamati ya Maadili

Mwenyekiti Kamati ya Huduma, Afya na Elimu.
Mwakilishi Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
Meya akikabidhiwa kombe la Mshindi wa Jumla katika Manispaa za mikoa ya kanda ya Mashiriki ambalo Manispaa ya Kinondoni iliitwaa wakati wa Maonyesho ya NaneNane. Anayemkabidhi ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hadija Hamza.
Meya Songoro Mnyonge akifunga kikao hicho, akihitimisha kupaza sauti juu ya Waziri Dk. Ndumbalo kusimamisha ujenzi wa shule ya Msingi uliokuwa umeanza kufanywa na Manispaa eneo la Panga, Tegeta, Kata ya Wazo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages