Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwaongoza Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate (kushoto) na Katibu wa itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla wakiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Kyerwa, Kagera Agosti 8, 2024.
''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
Akihutubia katika mkutano huo, Dk. Nchimbi ameyatakia heri wakulima katika Maadhimisho ya Siku ya Wakulima NaneNane alipowakuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara wilayani Kyerwa, Kagera leo gosti 8, 2024.
Dk Nchimbi ameiagiza serikali kuendelea kusimamia bei bora za mazao na kusambaza kwa wakati pembejeo.
Dk Nchimbi ameanza ziara leo katika Wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambapo amefanya mikutano ya hadhara.ikiwa nimwendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Kagera iliyoanzia eneo la Nyakanazi baada ya kumaliza ziara ya siku tatu mkoani Kigoma. Akimaliza ziara Kagera ataendelea na ziara katika mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa ambayo ni; Geita, Mara na Mwanza.
Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Dk Nchimbi akihutubia katika mkutano huo na kuwaomba wananchi kujisajili kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura na kuipigia kura CCM wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Wananchi wa Kyerwa wakinyoosha mikono kukubali kuipatia ushindi CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kumpatia kura Samia Suluhu Hassan.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla akizungumza wakati wa mkutano huo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇