LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2024

DK NCHIMBI AWATAKA VIONGOZI KUWATUMIKIA WANANCHI KWA MAPENZI YAO YOTE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK. Emmanuel Nchimbi akisikiliza wakati Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Evance Mallasa akijibu baadhi ya kero za wananchi zilizotolewa kwake katika mkutano Kakonko mjini Agosti 6, 2024.

                                                    .............

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK. Emmanuel Nchimbi amewataka viongozi kuwa na moyo wa kuwatumikia wananchi kwa  mapenzi yao yote.


Amelihimiza hilo aliposimama kuwasalimia wananchi wilayani Kakonko wakati wa.ziara yake mkoani Kigoma. Agosti 6, 2024. Alianza ziara ya siku 3  katika Mkoa huo Agosti 4, 2024 na kuhitimishwa leo wilayani Kakonko.


DK Nchimbi amewaomba wananchi waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za.Mitaa Novemba mwaka huu kwa kuwachagua viongozi watakao watumikia vyema.


Baada ya leo asubuhi kufanya ziara katika Wilaya ya Kibondo na Kakonko, msafara wa Dk Nchimbi  umeelekea wilayani Biharamulo mkoani Kagera kuendelea na ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni; Kagera, Geita, Mara na Mwanza.


Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2025.


Katika ziara hiyo Dk. Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Oganaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.




Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Andengenye akifurahia hotuba ya Dk Nchimbi.

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Dk Florence Samizi akifurahia hotuba ya Dk Nchimbi wilayani Kakonko.

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA -0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages