Ziara Ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK. Emmanuel Nchimbi imetua katika Wilaya ya Kibondo ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Kigoma.iliyoanza Agosti 4, 2024.
Akiwa katika Wilaya hiyo Dk Nchimbi anatarajia kufanya mkutano na kuwasalimia wananchi eneo la Kakonko na baadaye msafara wake utaelekea Nyakanazi, wilayani Biharamulo mkoani Kagera kuendelea na ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni; Kagera, Geita, Mara na Mwanza.
Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid
Dk Nchimbi akizungumza na wananchi wa Kibondo,
Dk Nchimbi akizungumza jambo na chipukizi wa CCM.








No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇