Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi na msafara wake wataendelea na ziara leo katika Wilaya ya Misenyi ambapo atafanya mkutano wa hadhara.
Akiwa njiani kuekekea Bukoba mjini, atasimama kusalimia wananchi eneo la Katoma.
Dk. Nchimbi anaendekea na ziara yake Mkoa wa Kagera na hadi sasa ameshafanya ya mikutano ya hadhara na kusalimia wananchi katika miji ya Nyakanazi, Biharamulo, Ngara, Kyerwa na Karagwe.
Katika mikutano yake hiyo, amepongeza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 ambapo serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imepeleka sh. Tril. 12 za maendeleo katika Mkoa huo.
DK Nchimbi ametatua baadhi ya kero za wananchi ikiwemo utata wa upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulifanyia kazi haraka.
Amemwagiza Waziri wa Maji, Jumla Aweso kwenda Kijiji Cha Makunazi Ngara na Kyerwa kutatua changamoto ya maji lakini pia ameitaka serikali kuendelea kusimamia ya mazao na kusambaza pembenjeo kwa wakati Ili wananchi wapate tija.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇