LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 12, 2024

DK NCHIMBI: ANGALIENI UWEZEKANO WA VIONGOZI WA CHADEMA KUWAACHIA HURU



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM), kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo amemuomba Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni kwamba waone uwezekano wa  viongozi wa  Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) waliokamatwa Mbeya kuachiwa huru ili apate wasaa wa kuzungumza nao  kwa vile CCM inaamini kwamba kuzungumza nao ni jambo zuri kabla ya sheria kufuata mkondo wake.upatikane muafaka.


Balozi Nchimbi amezungumza hayo leo Agosti 12, 2024, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Katoro, mkoani Geita akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya siku 3, mkoani humo, aliyoanza Agosti 11, 2024.


“Nimesikia kule Mbeya kulikuwa na tafrani kidogo kati ya Chadema na Polisi, na sisi kwa staili ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, anapenda sana mambo yawe yanamalizwa kwa kuzungumzwa, badala ya kukimbizana kimbizana kila mahali.

“Sasa nikasema kwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa, mambo ya sheria, siyo ya kutolea maelekezo Kiongozi wa Chama cha siasa, au siyo? Lakini nitumie nafasi hii, mwambie Waziri wako, kwamba tunaomba, muone uwezekano wale viongozi wa vyama vya siasa waachiliwe. 


Balozi Nchimbi amezungumza hayo leo Agosti 12, 2024, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Katoro, mkoani Geita akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya siku 3, mkoani humo, aliyoanza Agosti 11, 2024.


Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri Sillo ameshukuru kupokea maelekezo hayo na kuahidi watayafanyia kazi haraka.



 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages