LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 20, 2024

DIWANI MICHAEL URIO ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA NAIBU MEYA, KINONDONI, LEO

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michael Urio, amechaguliwa kwa kishindo kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kuchukua nafasi ya Josephat Rwegasila aliyemaliza muda wake.

Urio amechaguliwa kwa kura zote 21 za ndio akiwa mgombea pekee katika uchaguzi huo ulifanyika leo Agosti 2024 kwenye Ukumbi wa Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kumkaribisha Urio baada ya kumtangaza, Meya Manispaa ya wa Kinondoni Songoro Mnyonge ameahidi kumpa ushirikiano  wa dhati katika kazi zote watakazofanya.

“Urio karibu ufanye kazi, umeahidi utanisaidia naomba unisaidie. Kawaunganishe madiwani wakusaidie,” amesema Songoro.

Kwa upande wake, Urio amewashukuru madiwani wenzake na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano katika kipindi alichopewa na kufikia malengo waliyokusudia.

“Naikishukuru chama changu (Chama Cha Mapinduzi-CCM), ambacho ndicho kilichonilea, sijawahi kufanya siasa kwenye chama kingine. Nawashukuru sana viongozi wangu kuanzia wa shina hadi Taifa,  hasa Mwenyekiti wa Chama Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,” amesema Urio.

Miongoni mwa  changamoto ambazo Urio ameahidi kuhakikisha zinatatuliwa ni hali ya miundombinu ya barabara hasa katika jimbo la Kawe.

“Jimbo la Kawe tuna changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara na toka mvua zimenyesha barabara nyingi hazipitiki,” ameeleza Naibu Meya huyo. Kwa mujibu wa utaratibu, uchaguzi mwingine wa kawaida wa Naibu Meya utafanyika Oktoba, 2025.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akimpongeza Naibu Meya wa Manispaa hiyo Michael Urio baada ya kuchaguliwa leo Agosti 20,2024. Kulia ni aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi huo Charles Lawisso.

Mwanzo👇

Meya wa Maispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akifungua kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Meya Songozo Mnyonge akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinodoni
Charles Lawisso.wakati wa kikao hicho.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Munhu Baba, Baba Halisi (mwenye vazi jeupe- kulia),akiwa kwenye kikao hicho kwa kualikwa.
Waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkuruhenzi wa manispaa akitangaza agenda za kikao hicho.
Meya Songoro Mnyonge akiendelea kuongoza kikao hicho.
Urio akiomba kura.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa akiendesha Uchaguzi
Meya akipigakura kuchagua Naibu Meya.
Urio akipigakura kujichagua.
Madiwani wakipigakura.
Urio akishiriki kuhesabu kura.
Baba Halisi akipiga makofi baada ya matokeo kutangazwa.
Watu ukumbini wakiwa wamesimama baada ya matokeo kutangazwa.
Meya Songoro Mnyonge akimkaribisha Urio kuketi meza kuu.
Meya Songozo Mnyonge akikaribisha baadhi ya waalikwa.
Baba Halisi akiwa amesimama kujitamulisha. "Baba Halisi ni jina langu, siyo cheo", akasema.
Urio akitoa neno la shukurani.
Meya akiendelea kuongoza kikao hicho.
Meya Songoro akiteta jambo na Naibu Urio kabla ya kuhitimisha kikao.
Meya akihitimisha kikao hicho.
Meya akitoka ukumbini baada ya kuhitimisha kikao hicho.
Meye Songoro Mnyonge akiwa katika picha ya Kumbukumbu na Naibu Meya Urio baada ya kurejea ofisini. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa.
Meye Songoro Mnyonge akiwa katika picha ya Kumbukumbu na Naibu Meya Urio baada ya kurejea ofisini.
Wananchi waliokuwa wakifuatilia kikao hicho nje ya ukumbi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages