Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imebakiza asilimia mbilli (2) tu kukamilisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo inaelekeza hadi ifikapo mwaka 2025 utoaji huduma ya maji wa mamlaka hiyo uwe umefikia asilimia 95.
Akizungumza leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Mkama Bwire, amesema hadi sasa (2024) Dawasa imeweza kufikisha huduma kwa asilimai 93 katika Mikoa yote 23 ya huduma, ikitegemea Mto Ruvu kuwa chanzo kikuu cha maji ambacho kinachangia asilimia 87 katika uzalishaji maji.
Mhandishi Bwire ametaja vyanzo vingine vya maji ambavyo Dawasa inavitengemea kuwa ni Mto Kizinga ambao unachangia asilimia mbili na Visima vilivyopo Kimbiji, Kigamboni.
Amesema bado Dawasa inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha mtandao wa kiliomita 7,087 unaotoa huduma unakuwa na ufanisi mkubwa na kuleta matokeo chanya.
" Tunaendelea kuboresha maeneo ya kutoa huduma ya maji takribani mikoa 23 ya kihuduma, lakini ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatutaka ifikapo mwaka 2025 tuwe wamefikisha asilimia 95 ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi", amesema Mhandisi Bwire.
Ameeleza kuwa kwa sasa maeneo mengi yanapata huduma ya maji muda wote, lakini maeneo mengine wapo katika hatua ya kufikisha huduma kwa kusambaza mtandao wa mabomba na kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama.
“Ukienda maeneo ya kigamboni kuna maji ya kutosha, kinachotakiwa kwa sasa ni kuongeza kasi ya uzambazaji wa mtandao wa mabomba katika maeneo yote yenye changamoto” amesema Mhandisi Bwire.
Mhandisi Bwire amesema kuwa kuna jumla ya matanki 138 yenye uwezo wa kuifadhi maji lita 183,649,000 na kuweza kutoa huduma kwa masaa yasiyopungua sita.
Amesema kutokana na uhitaji bado wanahitaji nguvu kutoka sekta binafsi ya kuongeza vyanzo vya maji, huku akieleza kuwa hivi karibuni wanatarajia kupata vyanzo vingine kutoka Mto Rufiji na Bwawa la Kidunda.
Mhandisi Bwire amesema ujenzi wa Bwawa la Kidunda utaboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi kwa kuhakikisha yanapatikana muda wote katika Mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani.
Amesema ujenzi wa Bwawa Kidunda unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita unatarajia kutumia zaidi ya sh. bilioni 300 ambao unatekelezwa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Sino Hydro Corporation ya China.
“Kukamilika kwa mradi wa kidunda utawezesha mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kuzalisha jumla ya lita milioni 466 kwa siku na kuzalisha maji muda wote na kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo” amesema Mhandisi Bwire.
Mhandisi Bwire amesema pamoja na kutoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam, pia wanatoa huduma ya maji baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Tanga, Morogoro na Pwani.
Afisa Uhusiano na Mawsiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri akifanya utambulisho na kumkaribisha kuzungumza, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire, katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi hiyo, leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire akifafanua jambo wakati akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wahariri wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano wa DAWASA Everlasting Lyaro akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Balile akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam.







No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇