LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 28, 2024

WANANCHI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA HOTUBA YA DK NCHIMBI MTWARA


 

Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba makini ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mtwara wakati wa ziara ya kikazi iliyoanza leo Julai 28, 2024 mkoani Mtwara.

Kabla ya mkutano huo mkubwa wa hadhara, Dk Nchimbi alizuru kaburi la Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa katika Kijiji cha Lupaso, pamoja na kufanya mkutano na viongozi wa CCM wa Wilaya ya wilayani Masasi.

Dk. Nchimbi akihutubiwa katika mkutano huo wa hadhara ambapo yeye pamoja na viongozi wengine wa CCM walisikiliza na kutatua kero za wananchi.

Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.














 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages