Na Victor Makinda,
Wafugaji nchini wameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyoelekeza nguvu kuboresha sekta ya mifugo.
Hayo yameelezwa leo mjini Igunga mkoani Tabora na Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) , Mrida Mshota wakati alipotembelea mnada wa mifugo wilayani hapa.
Mshota amesema kuwa kwa muda wa miaka mitatu tangu Rais Samia aingie madarakani Machi 19, 2021 maisha ya wafugaji nchini yamekuwa bora zaidi kwa kuwa serikali imeirishwa sekta ya mifugo kwa kuiwezesha katika maeneo ya pembejea, malisho, mikopo na masoko yenye tija.
"Kwa miaka mitatu ya Rais Samia madarakani bajeti ya Wizara ya Mifugo imepanda kutoka Shilingi Bilioni 169 mpaka Bilioni 460." Amesema Mshota.
Amesema kuwa jumla ya wafugaji 8413 wamepatiwa mikopo mikubwa kutoka kwenye mabenk, iliyowasaidia kuboresha shughuli.za ufugaji kutoka ufugaji wa kimazoea wa zamani na kuanza kutumia mbinu bora za ufugaji wa kisasa.
Akizungumzia kuhusu pembejeo za mifugo amesema kuwa kwa mwaka 2023-24 serikali imetoa jumla ya lita 56 elfu zenye thamani ya Shilingi Bil 2.6 kwa wafugaji kote nchini.
Kuhusu wafugaji kumilikishwa ardhi, Mshoto amesema kuwa jumla ya hekta Milion 3.5 zimekwisha pimwa na kumilikishwa wafugaji maeneo mbali mbali nchini hatua iliyosaidia kupunguza migogori baina yao na wakulima.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita katika kuonesha inajali maslahi ya wafugaji nchini imechimba jumla ya mabwawa 20 ya kunyweshea mifugo sambamba na kuanzisha minada mipya ya mifugo 15 kote nchini.
Mshota amepongeza mpango wa serikali kupitia Wizara ya Mifugo wa kutenga Shilingi Bil 29 kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya kuchanja mifugo.
" Sisi CCWT na wafugaji kwa ujumla tuna furaha kubwa na tunatamani Rais Samia aongezewe muda mwingine ili maisha yetu yaendelee kuwa mazuri zaidi." Amesema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇