LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 24, 2024

UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA WATINGA KAGERA NA GEITA, KUANZA AGOSTI 5, 2024

Na Waandishi Maalum, Geita na Kagera
Mzunguko wa pili wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaojumuisha mkoa wa Geita na Kagera utaanza tarehe 5 hadi 11 Agosti, 2024 kwa  vituo kufunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Geita leo tarehe 24 Julai, 2024.
 
Mkutano kama huo mkoani Kagera umefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Juji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk. Mikutano hiyo inafanyika ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hiyo katika mikoa hiyo..
 
“Mzunguko wa pili wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utajumuisha mkoa huu wa Geita na Kagera ambapo uboreshaji utaanza tarehe 5 hadi 11 Agosti, 2024. Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Amesema, mikoa hiyo inafanya uboreshaji kwenye mzunguko wa pili baada ya mzunguko wa kwanza ambao uliumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora ambako uboreshaji umeanza tarehe 20 Julai, 2024 na unatarajiwa kukamilika tarehe 26 Julai, 2024.
 
Uzinduzi wa boreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ufanyika mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 na mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), uzinduzi ambao ulifanyika sanjari na kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa Uboreshaji kwenye mikoa hiyo mitatu ya Kigoma,Tabora na Katavi ambao unaendelea hadi tarehe 26 Julai, 2024.
 
Akizungumza mkoani Kagera, Mhe. Jaji Mbarouk amesisitiza kuwa kadi za wapiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi zijazo. Hivyo, amewataka wadau wa uchaguzi kwenye mkoa huo kuwaelimisha wapiga kura wenye kadi hizo wasiende kuboresha taarifa zao kwa kuwa zoezi hilo haliwahusu.
 
“Kwa mujibu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 kadi za mpiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 zenye jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi zijazo. Hivyo, zoezi hili la uboreshaji wa Daftari haliwahusu wapiga kura wenye kadi hizo,” Jaji Mbarouk amesema.
 
Akizungumzia teknolojia ya uandikishaji wa wapiga kura wakati wa kuwasilisha mada, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan amesisitiza kuwa wapiga kura wanaoboresha taarifa zao wanaweza kuanza mchakato wa awali kwa kutumia simu janja au kiswaswa na kompyuta kupitia mfumo ujulikanao kama Online Voters Registration System (OVRS) au kwa kubobya *152*00#, kisha namba 9 na kufuata maelekezo.
 
”Mtumiaji wa huduma hii, atatakiwa kufika kituo anachokusudia kujiandikisha ili akamilishe hatua za kupigwa picha, kuweka saini na kupatiwa kadi yake ya mpiga kura,” amesema Bw. Kailima.

Meza kuu ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile

 

Viongozi wa kimila ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchaguzi hivyo Tume iliwashirikisha viongozi hao kutoka Kagera.
Wadau kutoka makundi mbalimbali ya wanawake na vijana nao walishiriki.
Wahariri kutoka Vyomb0 vya habari nao walishiriki. 
Washiriki kutoka vyama vya siasa. 
Viongozi wa dini.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk akiongoza majadiliano wakati wa Mkutano huo.
Mdau akiuliza maswali na kutoa maoni yake.
 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile akifafanua jambo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages