LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2024

NJEZA AWAHAKIKISHIA WANANCHI KATA YA IKUKWA KUUNGANISHIWA UMEME

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Oran Njeza amewaeleza Wananchi  wa Kata ya Ikukwa kwamba Serikali ina mpango wa kuingiza  umeme nyumba kwa nyumba kwa sababu tayari lengo la kijiji kwa  kijiji limefanikiwa kwa 100%. 

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, ameanza ziara katika jimbo hilo yenye lengo la  kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhuisha uhai wa chama.

Njeza ahimiza wananchi wa kijiji cha Ikukwa na Simboya kwenda kuhakiki taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili muda ukifika wakashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa  Novemba 11, 2024

 


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages