Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, wakati alipowasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Baraza hilo, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi, Julai 3.2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………….
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza ufanyaji kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za Dini nchini ili kuendelea kujenga amani, umoja na mshikamano.
Amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizo ambao huleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.
“Tunashukuru tunapata ushauri, yapo mambo ambayo mnayafanya na kuiwezesha nchi hii iendelee, mshikamano wetu ndani ya nchi, umoja wetu ndio unaozaa utulivu na amani tuliyonayo”
Amesema hayo wakati akiwasilisha Salamu za Pongezi kutoka kwa Rais Dkt. Samia leo (Jumatano, Julai 03, 2024) kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kumpa ushirikiano wa dhati “wakati wote utakapokuwa na jambo ambalo unadhani Serikali inahitaji kushauriwa uwe huru na wakati wote unapoona kwamba unahitaji kuunganisha nguvu na Serikali, sisi tutakupa ushirikiano”
Ameongeza kuwa Serikali kwa upande wake imeshaagiza ushirikiano huo usiwe tu ngazi ya kitaifa bali uende hadi katika ngazi ya vitongoji “Tuendelee kuwa pamoja na kuja kwangu hapa nikuhakikishie tunaendelea kukupa ushirikiano”
Kwa upande wake Askofu Pisa amemshukuru Rais Dkt. Samia Kwa salamu za pongezi za kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa TEC
Uchaguzi wa viongozi wapya wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) uliohusisha nafasi za Rais, Makamu wa Rais na Katibu ulifanyika tarehe Juni 21, mwaka huu, ambao waliochaguliwa ni Mhashamu Wolfgang Pisa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi (Rais), Mhashamu Eusebius Nzigilwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda (Makamu wa Rais) na Padre Charles Kitima Padre wa Jimbo Katoliki la Singida (Katibu Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, wakati alipowasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Baraza hilo, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi, Julai 3.2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, wakati alipowasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Baraza hilo, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi, Julai 3.2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mti baada ya kuupanda, wakati alipowasili kwenye makazi ya Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, kuwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) mkoani Lindi, Julai 3.2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇