LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2024

KINANA AG'ATUKA UONGOZI CCM, DK. SAMIA ARIDHIA KWA MOYO MZITO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amejiuzulu Umakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia.

 "Ni kweli nilipokuomba utusaidia kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako", imesema taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Amos Makalla ikikariri sehemu ya majibu ya Dk. Samia kufuatia ombi la Kinana.

"Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika,

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu", amesma Makalla katika taarifa hiyo.




No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages