Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifungua Kikao cha Kibunge wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, Jijini New York, Marekani leo tarehe 16 Julai, 2024.
Kikao hiki kinaangazia lengo nambari 16 lenye kusisitiza Amani, Haki na Taasisi madhubuti. Aidha, namna ambavyo Mabunge yatasaidia kuzishauri na kuzisimamia Serikali zao katika kutimiza lengo hilo.
Mabunge yameshauriwa kujikita kwenye uwazi, usawa na uwajibikaji kama njia mojawapo ya kutimiza lengo linaloangaziwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇