LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 19, 2024

DK. SELELA KUIAGA LEO TIMU YA TANZANIA ITAKAYOSHIRIKI MICHUANO YA OLIMPIKI JIJINI PARIS, UFARANSA

Na Issa Michuzi, Mwambata wa Habari na Mawasiliaono, TOC
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Suleiman Selela, leo anatarajiwa kuiaga na kuikabidhi bendera timuyaTaifai itakayoshiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto inayoanza Ijumaa Julai 26 hadi Jumapili Agosti 11, 2024 jijini Paris na mijimingine 16 nchini Ufaransa.

Makamu wa rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Henry Tandau amesema hafla hiyo ya kuiaga na kuikabidhi bendera timu hiyo yenye jumla ya wanamichezo 15 watakaoiwakilishaTanzania katika michuano hiyo mwaka huu, itafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika Uwanjawa Benjamin William Mkapa jijini Dar es salaam.

Tandau amesema katika toleo hili la 33 la Michezo hiyo ya Olimpiki, kikosi cha Tanzania kitakuwa na nahodha mkimbiaji Alphonce Felix Simbu ambaye pamoja na mkimbiaji mwenzie Gabriel Geay watashiriki katika mbio za Marathon kwa wanaume.

Ametaja wengine kuwa ni wanariadha Jackline Juma Sakiluna Magdalena Crispin Shauri,  ambao watashiriki michuano ya Marathon kwa wanawake.

Pia amewataja waogeleaji wawili, Sophia Anisa Latiff atakayechuana mita 50 freestyle, kategori ya wanawake na Collins Phillip Saliboko atakayecheza mita 100 freestyle kwa wanaume. Mwanamichezo wa saba ni Andrew Thomas Mlugu, atayeshiriki katika mashindano ya mchezo wa Judo,

Tandau amesema timu hiyo itaambatana na makocha watatu wafani hizo tatu za michezo, daktari watimu, Mwambata wa Mawasiliano na Habari pamoja na maafisa wawili kutoka TOC.

Zaidi yawanamichezo10,500 kutoka mataifa 206 wanatarajiwa kushiriki katika matukio 329, na fani 45  tofauti za michezo. Kwa mara ya kwanza kila jinsia itawakilishwa nawanamichezo 5,250.

Katika michezo hiyo kutakuwepo na Breaking (ainaya breakdancing) ambayo itakuwa ikichezwa kwa mara ya kwanza kwenye Olimpiki, pamoja na kuteleza kwa ubao (Skateboarding) kupanda ukutana kuelea kwenye mawimbi (surfing)makubwayabahari.

Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza katika Michezo ya Olimpiki mwaka 1964 huko Tokyo, Japan, na toka wakati huo  imepeleka wanariadha kushiriki katika kila Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto isipokuwa ile iliyosusiwa mwaka 1976,  ila haijawahi kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi.

Mwaka huo wa 1976, nchi 29, nyingi zikiwa za Kiafrika, zilisusia Michezo ya Olympic iliyofanyika Montreal, Canada, baada ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kukataa kuipiga marufuku New Zealand, baada ya timu yake ya kitaifa ya raga (rugby) kuzuru Afrika Kusini mapema mwaka 1976 kinyume na wito wa Umoja wa Mataifa wa michezo ulioiwekea Afrika Kusini vikwazo kutokana na msimamo wao wa ubaguzi wara ngi.

Kamati ya Taifa ya Olimpiki ya Tanzania iliundwa mwaka1962, ilikushiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow, Scotland.  Mwaka1968  TOC ilitambuliwa rasmi na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).

Dk. Selela

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages