Na Bashir Nkoromo, Tegeta.
WATEKELEZA Sauti wa Kanisa Halisi walimuwakilisha vilivyo BABA HALISI, kwa kuongoza vema, Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na mamia ya Uzao (waumni) jana, 19 Tamuzi 1. Majira Halisi (Juni 9, 2024).
Ibada hiyo iliongozwa na Mtekeleza Sauti Amani Halisi wa Moyo Mmoja (Makao Makuu) akiwa na Watekeleza Sauti viongozi wakiwemo Fahari Halisi na Kanisa (mke wake), Utulivu Halisi Dk. Uelewa Halisi na Ubora Halisi.
Akiendesha Ibada hiyo Amani Halisi alionekana kuwasisimua washiriki wa Ibada hiyo ambayo aliongoza kwa Somo (sauti) ya 'Jicho la Moyo Halisi), akisema kwamba Jicho la Moyo Halisi ndilo linaloweza kuona na kupokea mema.
Akisisitiza, Amani Halisi alinogesha somo hilo kwa kumuita Mtekeleza Sauti Moja (Utulivu Halisi) na kumwambia afumbe macho, kisha akamwambia apokee chupa ya Damu safi nyeupe (maji), lakini akashindwa kuipokea kwa kuwa alikuwa haoni.
Kisha akamwambia afumbue macho, Utulivu Halisi alipofumbua macho Amani Halisi akamwambia apokee chm chupa ile, akaipikea.
"Mmeona alipokuwa amefumba macho hakuweza kuipokea, lakini alipofumbua macho akawa anaona ameweza kuipokea, hivyo ndivyo ilivyo. Sasa leo tunapokea Jicho la Moyo Halisi, tupate kuona sawasawa mema yote", akasema Amani Halisi.
Mbali na mahubiri, Ibada hiyo ilichangamshwa vilivyo na Waimbaji wa Sauti Moja Halisi ambao waliungurumisha nyimbo kadhaa mara kwa mara zilizowafanya Uzao kucheza bila kuchoka.
Katika Ibada hiyo, BABA HALISI hakuwepo, kwa alikuwa Jijini Mwanza ambako aliongoza Ibada kubwa ambako aliachilia sauti 'Kanisa limerejea kwenye barabara ya Sauti'
Mtekeleza Sauti Amani Halisi aliongoza Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa Halisi, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, jana.
Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Uzao akiandika kwenye daftari lake somo lililokuwa likitolewa na Amani Halisi kwenye Ibada hiyo.
Amani Halisi akimwambia Mtekeleza Sauti Moja avumbe macho wakati akitoa mfano wa 'Sauti ya Jicho la Moyo Halisi'.
"Pokea chupa hii...", akasema Amani Halisi, lakini Mtekeleza Sauti Moja akashindwa kupokea ka kuwa alikuwa amefumba macho, haoni.
Alipoambiwa tena apokee chupa akiwa amefumbua macho akaipokea!
Amani Halisi akiendelea kufafanua zaidi maana ya somo la 'Jicho la Moyo Halisi'.
Waimbaji wa Sauti Moja Halisi wakitumbuiza.
Uzao na atekeleza sauti wakicheza
Amani Halisi akiongoza shukurani.
Uzao wakipokea shukurani kwa shangwe.
Uzao wakipokea shukurani kwa shangwe.Watekeleza sauti Ubora Halisi kutoka mkoa wa Pwani, Utulivu Halisi na Dk. Uelewa Halisi wakifurahia jambo baada ya Ibada.
Baadhi ya Uzao wakitangulia kuondoka baada ya Ibada hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇