LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 19, 2024

RAIS SAMIA AAGIZA HADI DISEMBA TAASISI ZA SERIKALI ZIWE ZIMEVILIPA VYOMBO VYA HABARI MADENI YOTE YALIYOHAKIKIWA

Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mambo mengine ameeleekeza kuwa ifikapo Disemba mwaka huu 2024, madeni yote ambayo vyombo vya habari vinazidai Taasisi mbalimbali za serika mbayo yamehakikiwa yawe yamelipwa.

Rais amesema hayo akihutubia baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Kutathimini Utendaji na Hali ya Uchumi katika vyombo vya habari nchini, wakati akifungua Kongamano la Maendeelo ya Sekta ya Habari nchini kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Juni 18, 2024.

Tume hiyo iliundwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, Januari 24, 2023 ikiwa ni maelekezo ya Rais Samia  kumtaka waziri huyo kushughulikia suala la uchumi kwenye vyombo vya habari.

Aidha Rais Samia amevitaka vyombo vya habari kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya kiteknolojia katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii, pia kufichua maovu na kutowajibika kunakofanywa na baadhi ya Watumishi na Watendaji wa Serikali.

Rais amesema kazi ya vyombo vya habari ni kutoa mrejesho wa hisia na mtazamo wa wananchi kwa Serikali yao, na kwa ujumla, vikijikita katika kufanya kazi ya kuelimisha na kukuza demokrasia, akisisitiza kuwa masuala hayo yanayoifanya Serikali kujenga na kuimarisha uhusiano mwema na vyombo vya habari.

“Vyombo vya habari sio mshindani wa Serikali bali ni mdau na mshiriki muhimu wa mambo yanayotendwa na Serikali, hivyo Serikali itaendelea kuweka mifumo mizuri ya Kisera, Kisheria na Kitaasisi, katika kuimarisha uhuru na mazingira ya kazi kwa vyombo vya habari.” amefafanua.

 

Rais amesema Serikali itaendelea kuweka mifumo ya kisera na kisheria katika kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa ufanisi.

 

Kauli mbiu “Jenga Mustakabali endelevu kwenye sekta ya habari katika zama za kidijitali”, Rais Dkt. Samia amesema kuwa vyombo vya habari sio mshindani wa serikali bali ni mdau ni mshiriki muhimu wa shughuli za serikali.

Amesema kuwa vyombo vya habari ni muhimu kulisemea Taifa mambo mazuri, lakini kuna baadhi ya waandishi wahabari na vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari mbaya za kulitangaza Taifa.

Amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa kuripoti habari za taifa kwa weledi na kutangaza Maendeleo yaliyofikiwa.

“Nikienda Nchi za wenzetu napongezwa kwa kazi nzuri inayofanywa kwa kusimamia sekta ya habari, lakini kuna baadhi ya wanahabari hawaoni mazuri yanayafanywa na serikali”amesema Rais Dkt. Samia.

Ameeleza kuwa vyombo vya habari vikifanya kazi yake kwa uhuru vinagusa kila pembe ya taifa na kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya teknolojia, kufichua maovu na kusaidia viongozi kupata mrejesho.

Rais Dkt. Samia amesema kuwa uhusiano kati ya serikali na vyombo vya habari unazidi kuimarika, huku akibainisha kuwa ripoti za kimataifa zikionesha kuimarika kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini.


Aidha Rais Dk.Samia amesikitishwa na tukio la mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Asmiwe Novath mwenye umri wa miaka miwili na miezi sita ambaye aliibiwa nyumbani kwao Mkoani Kagera na baadaye kupatikana akiwa amefarikia dunia huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimenyofolewa,

 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, amesema kuwa Tanzania haijafika katika uhuru wa habari unaoutarajiwa angalau ipo katika hatua tofauti na siku za nyuma.

Amesema kuwa hatua hiyo ni mageuzi ya usimamizi katika sekta ya utangazaji na mapitio ya sera na kanuni ambayo misingi wake ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia.

” Lengo la kongamano hili ni kutathmini sekta ya habari na kuweka mikakati tunakokwenda na kongamano hili ambalo ni la pili kufanyika kutakuwa na mada mbalimbali na kujadili kuondoka na maadhimio,” amesema Nnauye.
















 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages