LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 5, 2024

MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA WAIBUA SHANGWE ZA WANANCHI MHERULE KILOMBERO

NA VICTOR MAKINDA: IFAKARA, MOROGORO

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kilombero, Mhandisi Florence Mlelwa.

Adha ya upatikanaji wa maji safi na salama, iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha Mherule, kata ya Mwanya Tarafa ya Mang’ula wilayani Kilombero mkoani Morogoro, imebaki historia baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama ya kunywa kijijini hapo.

Wakizungumza kwa furaha na CCM Digital, wananchi wa kijiji hicho walisema kuwa wamefurahia mno kutekelezwa mradi huo wa maji ambao licha ya kuwatua ndoo kichwani akina mama, pia utakuwaepushia magonjwa ya mlipuko yaliyokuwa yakiwapata kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salama.

Shamsia Seleman, mwananchi wa kijiji hicho akizungumza kwa niaba ya wenzake anasema kuwa awali hapakuwa na  maji safi na salama kijijini hapo ambapo walikuwa wanakunywa maji kutoka kwenye mabwawa  na vidimbwi yaliyokuwa yakiwasababishia magonjwa ya mlipuko ya tumbo ya mara kwa mara.

“ Tunamshuru Rais Samia Suluhu Hassan , kwa kututua ndoo kichwani sisi wananchi wa Mherule kwani tulikuwa tunapata shida kubwa ya maji na magonjwa ya tumbo ya mara kwa mara”. Anasema.


 Anasema kuwa uwepo wa mradi huo kijijini hapo utawapa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo kwa kuwa awali walikuwa wakitumia muda mrefu kutafuta maji.

 Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mherule, Mustapha Chapchap anasema kuwa kijiji hicho chenye wakazi 2400 hakijawahi kupata huduma ya maji ya bomba tangu Tanganyika ipate uhuru mwaka 1961  hivyo anaishukru serikali ya awamu ya sita kusikia kilio chao na kuwapelekea mradi wa maji safi na salama.

Akizungumza mapema leo na CCM Digital, kuhusu  uitekelezaji wa mradi huo, Mneneja wa RUWASA wilaya ya Kilombero, Injinia Frorence Mlelwa, anasema  kuwa jumla ya Shilingi  542,989, 000  zimetumika kutekeleza mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 85 ambapo unatarajiwa kukabidhiwa rasmi Octaba mwaka huu ukiwa tayari umeanza kunufaisha wananchi.

“Ruwasa Kilombero, tumetekeleza ujenzi wa mradi wa maji safi na salama kijiji cha Mherule, ambao umehusisha  uchimbaji wa kisima kirefu, uwekaji wa pampu ya umeme,ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo kuihifadhi lita 100, 000  sambamba na vituo vya kuchotea maji (DP) 8 vinavyotoa maji safi na salama ambayo mwananchi haitaji kuyachemsha kabla ya kunywa”. Anasema Injinia Mlelwa.

 Anaongeza kuwa vituo vyote vya kuchotea maji vimewekewa mfumo wa malipo ya kabla kwa kutumia mfumo wa   kadi janja (smart card).

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages