LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 26, 2024

DK. MWINYI AZUNGUMZA NA WATENDAJI JUMUIYA ZA CCM, ASISITIZA KASI YA MAENDELEO ITAONGEZEKA ZAIDI YA KABLA YA UCHAGUZI MKUU

Ikulu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema  Serikali itaongeza kasi zaidi  kukamilisha miradi ya maendeleo kupitia ilani ya utekelezaji ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 kabla ya uchaguzi mkuu. 


Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 26 Juni 2024, Ikulu Zanzibar  alipokutana na kuzungumza na Watendaji wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa akiwemo Katibu Mkuu UWT Taifa Suzan Kunambi, Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar  Abdi Mahmoud, Naibu Katibu Mkuu Wazazi Zanzibar  Ali Issa Ali, na Naibu Katibu Mkuu UWT Zanzibar  Tunu Kondo


Nao Watendaji wa Jumuiya hizo wamempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na kuvuka baadhi ya sekta mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages