NA VICTOR MAKINDA: IFAKARA, KILOMBERO.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kilombero, Florence Mlelwa.
Katika kuhakikisha kuwa lengo la
serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuwafikishia maji safi na salama asilimia 85 ya wananchi waishio
vijijiji na 95 waishio mijini mpaka kufikia mwaka 2025 linatimia, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini
(RUWASA) wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, umepanga kutumia jumla ya Shilingi 4,854,177,086.35
kutekeleza miradi ya maji katika mwaka
mpya wa fedha unaotarajiwa kuanza Julai Mosi 2024-2025.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ifakara mji, Kassim Nakapala, akichangia katika kikao cha wadau wa maji.
Hayo
yamebainishwa leo mjini Ifakara, Wilayani Kilombero na Meneja wa wa RUWASA,
wilaya ya Kilombero, Mhandisi Florence Mlelwa, wakati akitoa taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya maji kwenye mkutano wa wadau wa maji uliolenga kujadili changamoto na kutafutia ufumbuzi.
Mlelwa
amesema kuwa katika mwaka ujao wa fedha unaotarajia kuanza Julai Mosi 2024/2025
wakala huo umepanga kutekeleza Miradi 6 ya Maji sambamba na kukamilisha ujenzi wa miradi ya maji ya Mbingu- Igima, na Mherule.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, Injinia Florence Mlelwa akizungumza na wadau wa mji.
“ Mwaka wa fedha 2024/2025 RUWASA Kilombero imepanga
kutekeleza Miradi 6 ya Maji katika Vijiji vya Mofu - Ihanga, Lugala,
Nakaguru, Mgugwe – Chisano na Ngalimila sambamba na Uchimbaji wa visima 10.
Mlelwa alivitaja
visima vinavyotarajiwa kuchimbwa kuwa ni kisima cha Ipinde, Lumumwe na Ngalimila. Vingine ni Ikwambi, Kalenga, Miyomboni, Msita Ibaku, Iduindembo na Kitete.

Wadau wa maji wakifuatlia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyotolewa na Meneja wa RUWASA wilaya ya Kilombero.
Anaongeza kusema kuwa kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2022 Wilaya Kilombero inakadiriwa kuwa na watu 582,960, ikiwa watu
199,641 wapo katika eneo la Ifakara Mji ambao wanahudumiwa na Mamlaka ya Maji
na Usafi wa Mazingira (IFAUWASA) huku
RUWASA inawahudumia watu 383,319 waishio vijijini ambao wanaopata
maji safi na salama ni 297,838 sawa
na asilimia 77.7%.
Akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa maji, Mkuu wa
Wilaya ya Kilomero, Dunstun Kyobya alipongeza kazi kubwa zinazofanywa na RUWASA
wilayani humo, huku akiziagiza taasisi zote zinadaiwa bili za maji kulipa
haraka ili kuiwezesha RUWASA kutekeleza majukumu yake kiufanisi.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇