NA VICTOR MAKINDA: KILOMBERO, MOROGORO.Imeelezwa kuwa watendaji wa vijiji na kata, wana nafasi kubwa ya kuisaidia Halmasahauri zao kukuza makusanyo ya kodi na ushuru mbali mbali, ikiwa tu watendaji wa vijini na kata watakuwa na moyo wa kujituma, bidii na ubunifu wa kushirikisha wananchi.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwaya, Halmashauri ya Ifakara Mji, Wilayani Kiombero Mkoani Morogor,o Acley Muhenga (pichani), wakati akizungumza na CCM Blog ofisini kwake mapema leo.
Muhenga ambaye amepata tuzo za ushindi wa ufanyakazi bora mara 11 mfululizo ikiwemo
mwaka huu, anasema kuwa watendaji wanapaswa kutanguliza uzalendo katika kutekeleza majukumu yao hasa kwenye ukusanyaji wa mapato ambayo ndiyo msingi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
"Mapato ni chukizo kwa binadamu, lakini mimi ninapambana nalo". Anasema.
Mhenga anasema kila anapopelekwa kwenye kuhudumu nafasi yake ya utendaji amekuwa akikuza mapato kwa asilimia kubwa, hali inayowarahisishia kazi wakurugunzi wa Halmashauru kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya ustawi wa wananchi.
Ponyeza hapa kuona zaidi
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇