LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 22, 2024

WAZIRI MAVUNDE AFUNGUA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YA KANISA HALISI MJINI DODOMA, BABA HALISI AHIMIZA KUTAJIRISHANA, AKEMEA DHULUMA, KUSIMAMIANA MABEGANI.

Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog, Dodoma
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, BABA HALISI, amekemea tabia ya dhuluma na kukaliana mabegani, akisema tabia hiyo ndiyo chanzo cha taasisi nyingi, jamii na hata Kanisa kuanguka.

BABA HALISI amesema hayo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yalioanza Mei 21, 2024, yakifunguliwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde, katika ukumbi wa Polisi Jamii mjini Dodoma.

"Naomba mjue kwamba tunaoona wamefanikiwa siyo wengi wamefika hapo bila kudhulumu. Kwa hiyo kitu cha kwanza ninachotaka nisisitize sikipendi ni kudhulumiana wakati wa kuzalisha, mimi nachukia dhuluma kwa sababu imesababisha taasisi nyingi kuanguka na jamii na hata Kanisa kuharibika.

Kwa hiyo nitazungumza kwanza ubaya wa dhuluma na nitaonyesha tabia hiyo ilianzia wapi, ili sisi tunapoanza kwa vitu kama hivi (viwanda) alivyosema Waziri, tunapopewa mtaji kama huo tuhakikishe tunafanya kwa haki bila kudhulumiana", akasema BABA HALISI na kuongeza;

"Kuna mfumo ambao upo duniani, kwamba ili ufike mbali lazima usimame kwenye mabega ya wengine, unawakanyagia mabegani wasifike pale ulipofika, sisi tusifanye hivyo. Haya mafunzo tutakayopata hapa turuhusu na wengine wajifunze ili tuwe matajiri tukiwa wengi.

Hii ni kwa sababu ukiwa tajiri peke yako kijijini basi wewe ni masikini kuliko kijiji kizima kwa kuwa wengine watalazimika kuchukua vile ulivyonavyo mpaka vitaisha hadi utaona kwamba bora uwe tajiri lakini uruhusu na wengine ili wote muwe navyo".

Akifafanua ilikoanzia tabia ya kusimamiana mabega au kudhulumiana, BABA HALISI alisema; "ukiangalia kwenye kitabu mtiririko wa uumbaji utaona mtindo tabia hii ilianzia mbali.

Wa kwanza kuumbwa na Muumba siyo Adamu kama tulivyofundishwa, anaitwa Moyo wa Mwanzo. Huyu alivamiwa na nafsi ya uvamizi, ndiyo ikazuka tabia hii".

BABA HALISI akasema, ili kuepuka tabia ya dhuluma na kukanyaga mabega ya wengine, ni lazima kufuata mafundisho ya Muumba ambaye hufurahi zaidi kuona kila mmoja akizalisha kwa haki na siyo mtu kumlilia akimuomba.

"Ukiangalia  kwenye kitabu, furaha hasa ya Muumba siyo kutusikia tukiwa tunalia ili atusaidie, furaha yake ni kuona kila tunachokifanya tunakifanya kwa haki, na kila tunachokizalisha tunakizalisha kwa haki", akasema BABA HALISI.

BABA HALISI alimweleza Waziri Mavunde kwamba kwa takriban miaka saba amekufa akifundisha Kanisani habari ya kwamba Ibada ni Uzalishaji kwa haki, lakini haikuwa rahisi hata ndani ya Kanisa watu wakakaa pamoja na kufanya kama ilivyo sasa ambapo wameweza na bidhaa zikaonekana.

"Huu ni mwaka wa saba, nikifundisha haya. Tulianza 2018 nikifundisha kipengele hiki ndani ya Kanisa, lakini hata ndani ya Kanisa ilikuwa siyo rahisi watu watano au kumi wakakaa pamoja wakafanya kitu kikaonekana.

Nawashukuru sasa hata tukiwa pale Ibadani utakuta bidhaa zao zipo pale,  ukimaliza ibada ukijua nyumbani kwako huna sabuni unanunua palepale. Kwa hiyo nashukuru wanaweza wakakaa pamoja bidhaa zikaonekana namna hiyo", BABA HALISI akasema na kushukuru.

Akifungua mafunzo hayo, Waziri Mavunde alilipongeza Kanisa Halisi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Dodoma na Chuo cha Elimu kwa wote kwa kuandaa mafunzo hayo, na kusema, mafundisho ya BABA HALISI ya Ibada ni Uzalishaji yana tija kubwa kwa jamii ya Watanzania.

Katika kuonyesha kuunga mkono hatua ya kufanyika mafunzo hayo, Waziri Mavunde alitoa sh. milioni moja kuchangia sehemu ya gharama ya vyeti kwa washiriki 400 wa mafunzo hayo, gharama ya kila cheti ikiwa ni sh.15,000.

Mapema BABA HALISI alimwambia Waziri Mavunde kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ambayo Kanisa Halisi limekuwa likiyatoa kwenye vituo vyake mbali mbali vilivyopo ndani na nje ya Tanzanaia.

"Mheshimiwa Waziri mafunzo haya unayotufungulia  leo, ni mwendelezo wa Kanisa kuyatoa. Hadi sasa vituo vyetu mbalimbali mikoani na nchi za nje, vimeshafikiwa, Congo DRC ilikuwa mwezi uliopita wa Aprili mwaka huu (2024) ambako Mwalimu alikuwa huko, na Msumbuji nao wameomba kufikiwa hivi karibuni", akasema BABA HALISI.

Mafunzo hayo ambayo yatafikia tamati Mei 24, 2024, yameshirikisha washiriki 400 wakiwemo Wanajeshi kutoka Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la akiba (mgambo), vikundi vya vijana, kina mama kikiwemo kinachounga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na maafisa kutoka taasisi mbalimbali.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde akipewa maelezo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, BABA HALISI, kuhusu bidhaa mbalimbali, baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali Mei 21, 2024, katika Ukumbi wa Polisi Jamii, mjini Dodoma. Mafunzo hayo yameandaliwa na Kanisa hilo kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi Dodoma na Chuo cha Elimu kwa wote.
BABA HALISI akitoa utambulisho wa Kanisa Halisi kwa Waziri Mavunde kabla ya Waziri kufungua mafunzo hayo. Kulia ni MAMA HALISI.

Mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi (ACP) Mtalemwa, akifanya utambulisho na kumkaribisha Waziri Mavunde, kuzungumza na kufungua mafunzo hayo.
Waziri wa Madini Mavunde akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo hayo. Kulia ni BABA HALISI na MAMA HALSI.
BABA HALISI akifurahi baada ya kupongezwa na Waziri Mavunde kwa kuandaa mafunzo hayo.
BABA HALISI akimshukuru Waziri Mavunde baada ya kufungua mafunzo hayo.
MAMA HALISI akimshukuru Waziri Mavunde baada ya kufungua mafunzo hayo.
BABA HALISI akieleza kwa nini 'Ibada ni Uzalishaji'
BABA HALISI akifafanua zaidi kwa nini Kanisa Halisi linahimiza Ibada ni Uzalishaji. Kulia ni MAMA HALISI.
Waziri Mavunde akimpongeza BABA HALISI kwa kueleza kwa kina maana ya Ibada ni Uzalishaji.
Waziri Mavunde akitangaza kuchangia sh. milioni moja kwa ajili ya sehemu ya gharama ya vyeti watakavyopewa wahitimu.
Waziri Mavunde akikabidhi sh. milioni moja hizo kwa Mtekeleza Sauti wa Kanisa Halisi, Amani Halisi.

Washiriki mbalimbali wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo👇

Polisi, na washiriki wengine.
Polisi, Magereza, Uhamiaji na washiriki wengine.
Uhamiaji, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na washiriki wengine.
Polisi na washiriki wengine.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo. Kulia ni Mwalimu Saravai Izina na Mtekeleza Sauti Amani Halisi.
Uzao na Watekeleza Sauti wa Kanisa  wa Kanisa Halisi.
Washiriki wakiwa kwenye ufunfuzi wa mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Watekeleza Sauti wa Kanisa Halisi.
Mnara Mmoja Halisi na Dada Udhihihirisho Halisi.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Waziri Mavunde akipewa maelezo na BABA HALISI kuhusu bidhaa mbalimbali baada ya kufungua mafunzo hayo. Watatu ni Mwalimu Izina kutoka Chuo cha Elimu kwa wote.
Waziri Mavunde akitazama bidhaa zilizokuwa zikionyeshwa na Wajasiriamali, baada ya kufungua mafunzo hayo.
MAMA HALISI akimzawadia Waziri Mavunde mingoni mwa bidhaa za uzalishaji.

Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha ya kumbukumbu ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
BABA HALISI na MAMA HALISI wakimsindikiza waziri Mavunde baada ya kufungua mafunzo hayo.
Mtekeleza Sauti Amani Halisi akiongoza shukurani wakati akimkaribisha mwalimu Izina kuanza kutoa mafunzo hayo.
BABA HALISI na MAMA HALISI wakishiriki kusikiliza mafunzo.
Mwalimu Izina akitoa mafunzo hayo.

Mwalimu Izina akitoa mafunzo hayo. 

 ©2024 CCM Official Blog/ Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages