LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 24, 2024

SERIKALI YAVALIA NJUGA AGENDA YA USALAMA WA CHAKULA

 

NA VICTOR MAKINDA, MOROGORO

SERIKALI imeipa kipaumbele ajenda ya usalama wa chakula, ikizingatiwa dira ya kujilisha na kuwalisha wengine kibiashara sambamba na kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa wazi kwa kuuza chakula nje ikiwa ni mkakati wa kukamilisha mipango sita  inayotokana na Mipango ya Maendeleo Endelevu ya Milenia (SDGs) kwa lengo la kukomesha baa la njaa nchini kufikia mwaka 2030.

Mkurugenzi wa Masoko na Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Kilimo,  Gungu Mibavu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Masoko na Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu, kwenye mkutano wa wadau wa masuala ya usalama wa chakula (National Food system pathways roadmap and costed action plan) ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  kilimo na Cakula (FAO).

Mibavu alisema kuwa mpaka sasa chakula kilichopo  kinatosheleza nchi na kubakiwa na ziada na kwamba hiyo inaonesha ni njia ya sahihi ya kufikia malengo ya milenia yaliyokusudiwa.

Aliwataka wadau wa mkutano huo kujidhatiti na kuhakikisha wanatumia vizuri miaka sita iliyobakia ya kukamilisha malengo endelevu ya Maendeleo ya Milenia (SDGs) ya mwaka 2030 waliyojiwekea tangu mwaka 2021.

 

Alisema tayari wameshakwisha saini itifaki mbalimbali za kibiashara  kwenye kanda ikiwemo  SADEC, EAC inayohusu utekelezaji wa dira ya kujilisha wenyewe na kuwalisha wengine kibiashara, kuongeza uzalishaji wa ndani wa chakula.

Naye Mratibu wa Uhimilivu wa Mfumo ya Chakula kutoka Zanzibar, Sihaba Vuai,  alisema katika kuhakikisha wanafanya mageuzi ya kilimo wamejikita kwenye mifumo ya minyororo ya thamani 6 iliyopo kwenye mazao ya kipaumbele.

Vuai ambaye pia ni Mkurugenzi msadizi wa masuala ya sera aliyataja mazao hayo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na mazao ya kilimo, matunda, viungo, mifugo  huku mkazo ukiwa ni kujikita katika kuimarisha miundombinu ya uzalishaji katika kilimo cha umwagiliaji wa mpunga na mazao ya mbogamboga.

Mratibu wa uhimilivu wa mifumo ya chakula kutoka Zanzibar Sihaba Vuai

Aliongeza kusema  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa sasa ina mpango wa kushirikisha serikali za mitaa katika masuala ya kilimo na kuwezesha wilaya 10 kati ya 11 zilizopo Zanzibar kunufaika zaidi na kilimo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages