LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 21, 2024

 

POLISI, TCRA WATOA NENO KWA

WAANDISHI WA HABARI MITANDAONI

 

Ripota, CCM Blog, Dar es Salaam

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, amewataka waandishi wa habari za mtandaoni  kufuata sheria, kanuni na misingi ya habari wanapoandika kazi zao badala ya kuleta uchochezi.

Aidha amesema, ulinzi na usalama wa Mwandishi wa habari ni muhimu kwanza kuliko kitu kingine.

Akizungumza kwenye Kongamano la  Jumuiya ya Wanahabari Mitandaoni (JUMIKITA), kwenye Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, kuna kila sababu ya mwandishi kuwa balozi wa amani, umoja na utulivu kwa kuchambua habari kabla ya kuiandika.

Amesema waandishi wa habari wanatakiwa kuepuka habari za uchochezi zinazovuruga amani ya nchi lakini lengo la mwandishi ni kupata wasomaji wengi na kujikuta akiingia kwenye mgogoro na vyombo vya sheria.

Misime amesema: "Lazima mzingatie Sheria mbalimbali za habari, msiandike habari tu kwa kuwa ni habari, mkizingatia sheria, tutakuwa na mitandao mizuri itakayotupatia habari nzuri katika jamii."

Ameutaka uongozi wa JUMIKITA kusaidia kutoa elimu kwa wanahabari mtandaoni ili kudhibiti hali hiyo kama ambavyo Baraza la habari Tanzania limekuwa likifanya.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, Mkurugenzi wa Leseni katika Mamlaka hiyo, John Daffa amesema Tanzania ina watumiaji wa mitandao milioni 36 pamoja na vifaa ya kutumia interneti milioni20.

Amesema tukitumia majukwaa haya ya habari vizuri pamoja na mitandao kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kuingiza kipato.

Daffa amesema kama wanahabari mtandaoni wanapaswa kuzingatia usalama ikiwemo kutofungua link ambazo hawazifahamu sanjari na kutumia nywila ambayo ni ngumu mtu mwingine kuifahamu kirahisi.

 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages