LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 5, 2024

KOMREDI KINANA AWATOLEA UVIVU CHADEMA, LEO MJINI DODOMA

Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara Komredi Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dodoma leo tarehe 05 Mei 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma amesisitiza mambo yafuatayo juu ya Umoja wa Kitaifa.


1️⃣"Katika mizunguko yao (CHADEMA); wameituhuhumu Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mambo ya uongo. Hatukatai kukosolewa, kusahihishwa lakini hatukubali kushutumiwa kwa mambo ambayo hayapo au ya kutungwa."


2️⃣ "Kubwa walilolifanya (CHADEMA) katika mizunguko yao ni kujenga chuki/mifarakano miongoni mwa watanzania. Hiyo ndiyo ilikuwa ajenda yao kubwa."


3️⃣ "Hakuna mtu wa kutufarakanisha (watanzania), hayupo. Ninyi ni mashahidi; wapo (watu) waliojaribu, wenye madaraka, vyeo na vikundi mbalimbali waliotaka kuuvuruga Muungano, walifika mbali?, hapana."


4️⃣ "Wanasema (CHADEMA) Rais Samia ni mzanzibar na hana nia njema na sisi (Tanzania Bara); hayo maneno hayana ukweli hata kidogo. Watanzania kataeni sumu hiyo (sumu ya utengano) inayotaka kujengwa miongoni mwetu."


5️⃣ "Wametafuta namna ya kushughulika na Rais, wameangalia barabara zinakwenda vizuri, maji yanakwenda vizuri, huduma za jamii zinakwenda vizuri, makao makuu Dodoma yanajengwa, bwawa la umeme linafanyiwa kazi, wakasema hakuna pakutokea, mzanzibar huyu hafai. Tukatae kauli hiyo, tusimame na Rais Samia Suluhu Hassan, anafanya kazi nzuri."


6️⃣ "Kataeni juhudi zinazofanywa za kujenga chuki dhidi ya Rais"


7️⃣ "Tusisikilize hoja za reja reja, tusikilize hoja za msimu zinazotaka kutugawa."


8️⃣ "Ndugu zangu hawa, wanazunguka sio wana hoja!, wanazunguka na vihoja. Moja likishindikana wanakwenda jingine. CCM na serikali yake na hata Rais Samia hatukatai kukosolewa, sisi sio Malaika, tunakosea, hatukatai kusahihishwa. Lakini kukejeli, kudharau, kupeza hapana."


9️⃣ "Tukatae kugawanywa na kufarakanishwa; watu waje na hoja zenye mashiko kuondoa umaskini."


🔟 "Hoja ya majimbo ni ajenda ambayo CHADEMA wamekuwa nayo tangu kuzaliwa kwake na watanzania wameikataa. Moja ya sifa kubwa ya nchi yetu ni umoja wa kitaifa, ambao Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume wametujengea misingi ambayo ni imara sana. Ndugu zangu watanzania, endeleeni kuikataa (hoja ya kutaka kuigawa Tanzania katika mfumo wa majimbo)."


1️⃣1️⃣ "Watu wanatafuta uongozi, tutafute sisi (CCM), CHADEMA, ACT, CUF tutafute uongozi kwa hoja zinazosaidia wananchi, zinazoleta maendeleo, zinazopunguza umaskini, tusitafute hoja rahisi za kuchonganisha watu, kufarakanisha watu, za kuvunja umoja wetu." 


#CCMImara

#KaziIendelee

#TunaImaniNaSamia

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages