LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 20, 2024

KANISA HALISI, JESHI LA POLSI NA CHUO CHA ELIMU KWA WOTE, WAANDAA MAFUNZO KAMAMBE YA UJASIRIAMALI KUANZIA KESHO, MEI 21 HADI 24 JIJINI DODOMA

Na Bashir Nkoromo, CCM Official Blog
Katika kutekeleza kwa vitendo mafundisho ya 'Ibada ni Uzalishaji', Kanisa Halisi lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, limendaa mafunzo maalum ya Ujasiriamali yatakayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Polisi Jamii (PJ) Jijini Dodoma.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, BABA HALISI, amesema Mafunzo hayo ambayo Kanisa hilo limeyaandaa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Chuo cha Elimu kwa Wote, yataanza kesho Jumanne, Mei 21 hadi Mei 24, 2024.

BABA HALISI amewaalika watu wote hususan vijana na kina mama kuhudhuria mafunzo hayo ili kutekeleza kwa pamoja agizo la CHANZO HALISI (Muumba wa Vyote na yote) la 'Ibada ni Uzalishaji mali'. Huku akisisitiza kuwa yatakuwa ni mafunzo ya kiwango cha juu kwa kuwa yatatolewa na Walimu waliobobea katika fani zote za ujasiriamali.

Tafadhali soma Mwaliko ufuatao kuona mafunzo yatakayotolewa👇.



Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi na Vituo vyote vya Kanisa hilo Ndani na Nje ya Tanzania Baba Halisi.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages