Tanzania katika kujizatiti kunufaika kiuchumi na mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (CAN 2027), imezikaribisha Kampuni za Ufaransa kuja kuwekeza jijini Arusha kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo nyumba za malazi na kumbi za mikutano, ikiwa ni maandalizi.
Makaribisho hayo yametolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara, Uchumi, Nchi zinazozungumza Kifaransa na Wafaransa waishio nje ya nchi, Frank Reister, katika ofisi za Wizara jijini Paris, Ufaransa, leo Mei 15, 2024.
Tanzania inatarajia kuwa Mwenyeji mwenza wa Mashindano ya CAN 2027. Ufaransa kwa upande wao wameonesha nia ya kuwekeza ili kuwezesha Tanzania kuhudumia wageni watakaofika wakati wa mashindano hayo.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Riester pia amewakaribisha wafanyabiasha na wawekezaji wa Tanzania kuwekeza nchini Ufaransa akisema nchi hiyo imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Waziri Makamba ameishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kuendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo nchini Tanzania kwa kufadhiri miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo nishati, miundombinu ya usafirishaji, maji safi, kilimo na afya.
Mawaziri hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya biashara na uwekezaji ambapo, Mhe. Makamba ametumia fursa hiyo kuukaribisha Ujumbe wa Wafanyabiashara utakaongozwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ufaransa (MEDEF) unaotarajia kushiriki kwenye Jukwaa la Biashara linalotarajia kufanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Mei, 2024 jijini Dar es Salaam na Zanzibar.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January
Makamba akizungumza na Waziri wa Biashara za Nje, Uwekezaji, Nchi
zinazozungumza Kifaransa na Wafaransa Waishio Nje ya Nchi, Mhe. Franck
Riester katika ofisi za Wizara hiyo jijini Paris, Ufaransa tarehe 15
Mei, 2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Noel Kaganda.
![]() |
| Mheshimiwa Waziri Makamba akisalimiana na Mheshimiwa Waziri Riester baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo. |
![]() |
| Mheshimiwa Waziri Makamba akiteta jambo na Mheshimiwa Waziri Riester baada ya kuwasili ofisini za Wizara jijini Paris, Ufaransa. |
![]() |
| Mheshimiwa Waziri Makamba akikaribishwa na Mheshimiwa Waziri Riester baada ya kuwasili ofisini za Wizara hiyo jijini Paris, Ufaransa |
![]() |
| Mheshimiwa Waziri Makamba akisalimiana na maafisa walioambatana na Mheshimiwa Waziri Riester katika mazungumzo. |
![]() |
| Mazungumzo yakiendelea. |
![]() |
| Picha ya pamoja. |









No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇